105. Leo Shangwe Zitolewe
1. Leo shangwe zitolewe
shujaa atoka kufani.
Mtumishi wa Bwana huyu
aone kushinda kwake
/:Shangwe shangwe!
Shangwe, shangwe
zitolewe!
Imbeni Haleluya! :/
2. Mwana Kondoo amekuwa leo
simba mwenye nguvu.
Jiwe kubwa halimwezi,
kaburi lamfungukia.
Shangwe, shangwe …
3. Bwana Yesu umeshinda,
utupe uliyoteka:
Utengemano wa Mungu
uliopata vitani!
Shangwe, shangwe …
4. Yesu tunakutukuza,
twataka utugombee.
Tuweze kushinda nawe,
kwa kuwa sisi tu wako.
Shangwe, shangwe …
Comments
Post a Comment