Posts

Showing posts from May, 2025

1. Hosiana! Asifiwe

Hosiana! Asifiwe ajaye kwa Jina la Bwana! Hosiana mbinguni! Anakuja kwa Jina la Bwana, Anakuja kwa Jina la Bwana, Hosiana! Hosiana! Hosiana mbinguni! Hosiana mbinguni!

2. Hosiana, Mesiya

1. Hosiana Mesiya, aingia mjini kwake. Fagieni popote, zipambeni njia zote; Tandikeni maua, aingie na shangwe. 2. Hosiana Mwokozi! Njoo, twakungojea Bwana Tumepamba mioyo, twakukaribisha kwetu. Tunakufungulia, milango ya mioyo 3. Hosiana, ee Shujaa! Utusaidie sisi. Tuwe wako kwa kweli, tukutumikie vema. Kwani hutakubali watu wasiokutii. 4. Hosiana Mfalme mkuu!  Uingie kwetu hima! Uliyebarikiwa, Uingie mlango wetu. Hosiana, karibu! Bwana, njoo! Haleluya!

3. Sayuni, ufuhi!

1. Sayuni ufurahi.   Shangilia Yerusalemu!   Yuaja Mfalme wako,   mwenye amani kwako.   Sayuni ufurahi!   Shangilia Yerusalemu. 2. Hosiana Mesiya    Utubariki sasa.    Jenga ufalme wako    Ulimwenguni mwote.    Hosiana Mesiya    Utubariki sasa. 3. Hosiana pongezi!    Twakuamkia Bwana!    Kiti cha enzi yako    chasimama milele.    Hosiana pongezi!    Twakuamkia Bwana.

4. Fungua Milango Yote

1. Fungua milango yote,   yuaja Bwana wa mbingu.   Mfalme wa wafalme wote,   Mwokozi wa ulimwengu.     Atuletea uzima;   kwa hiyo tumwimbieni:   Tumsifuni Mungu,   aliyetuumba. 2. Ni mwenye haki na shujaa,    upole mwingi amevaa;    Rehema ni taji yake,    huruma ni fimbo yake:    Atuondolea shida.    Kwa hiyo tumwimbieni:    Tumsifuni Mungu,    Mwokozi wetu mkuu. 3. Miji na nchi huchipushwa,    afikako Mfalme huyu;    nayo mioyo huchekeshwa,    anayoingia Yesu.    Ndiye jua la furaha    linalotufurahisha.    Tumsifuni Mungu    mtunza mioyo yetu. 4. Fungua milango yote!    Tengenezeni mioyo!    Makuti yawe upole,    furaha, pendo, amani.    Mwokozi atawajia,    aleta raha, uzima.    Tumsifuni Mungu,    ni mwenye rehema. 5. Njoo, Mwokozi...

5. Nikulakije Vema

1. Nikulakije vema    Bwana wangu Yesu?    Wote wanakungoja    wapewe uzima.    Nuru yako ing’aze    hata moyo wangu.    Nijue mambo mema,    yakupendezayo. 2. Wamekutandikia    maua na nguo.    Nami nakuimbia    nyimbo za furaha.    Moyo ukupendeze    kwa sifa na nyimbo    ukakutumikie    siku zangu zote. 3. Umetoka mbinguni    ukawa maskini.    Ukaacha furaha    utupe uzima.    Na tuliponyang’anywa ufalme    na raha,    ukaja Mponya wetu     kuturudishia. 4. Nalifungwa na mwovu:    Ukanifungua.    Nikawa nimetwezwa,    ukanitukuza.    Ukanifanya mkubwa,    ukanipa mali,     zisizomalizika,    kwa kutu na wezi 5. Umenijia mimi,    sababu ya nini?    Sababu ya kupenda,    ...

6. Wakristo, Iwekeni

1. Wakristo, iwekeni    mioyo tayari.    Yesu awaingie,    ni Mwokozi wenu.     Mungu amemtuma    kwa neema na rehema,     atuletee sisi    uzima na nuru. 2. Mwokozi anakuja,    mlimieni njia!     Mioyo iwe safi     acheni matendo    yanayomchukiza.    Lijazwe kila bonde,    milima ipunguzwe    mioyoni mwenu. 3. Ukiwa mnyenyekevu,    wapendwa na Mungu.    Ukiwa na kiburi,     utaangamizwa.     Ukimtumikia,    Mungu kwa mwendo    mwema    umpendezao yeye,    Yesu akupenda.   4. Uniweke tayari    niliye maskini,    Ee Yesu siku hizi     Ingia moyoni,     ukinijia sasa.     Nami nitakusifu    kwa kinywa na moyo.

7. Moyo Wangu Sikiliza

1. Moyo wangu sikiliza,    habari njema hii,    ya wokovu mkubwa.    Sikia kuimba    kwao malaika na watu:    “Yesu azaliwa.” 2. Mponya amekuja leo     kutoka mbinguni,     aokoe watu.    Mungu wetu ameshuka,    akawa mwana mtu    kwa ajili yetu. 3. Na sasa yumo zizini,    aita: “njooni,    hima kwangu wote,     Nawaondolea ninyi     uchungu wowote,     muwe na furaha.” 4. Basi tumwendee hima     wakubwa wadogo,     njooni wote sasa!    Yule anayetupenda,     tumpende na sisi,     awe mwanga wetu. 5. Wenye shida na ukiwa njooni,    awape    neema yake Mungu,     Yeye ana mali nyingi,    dhahabu na fedha     za mioyo yenu. 6. Ninakaa ulimwenguni     lakini napenda  ...

8. Amekuja Mwokozi

1. K: /: Amekuja    W: Mwokozi. :/    K:  /: Ufalme wa juu karibu.    W: Amekuja Mwokozi.:/ 2. K: /: Geukeni    W: mioyo. :/     K:  /: Watatupwa wenye kiburi.    W: Geukeni mioyo. :/ 3. K  /: Shoka lipo    W: Shinani, :/     K:  /:Mti usiozaa wakatwa.    W: Shoka lipo shinani. :/ 4. K: /: Ana ungo    W: mkononi, :/     K: kupepeta ngano yake.     W: Ana ungo mkononi. :/ 5. K: /:Yatachomwa     W: Makapi, :/     K: Ngano            yawekwa chanjani.    W: yatachomwa makapi :/ 6. K: /:Nabatiza W: kwa maji, :/     K: Yeye, hubatiza kwa Roho.     W: Nabatiza kwa maji. :/ 7. K: /:Mbele yake sifai, :/     W: Sifai, :/    K: Kumfungulia viatu,     W: Mbele yake sifai. :/   8. K: /: Elekea ...

9. Faraja, Tumaini Langu

1. Faraja, tumaini langu     usiniache gizani.    Moyo ni wazi kukungoja,    Ee Yesu uniingie.     Furaha ya mbingu na    nchi, Mwana Adamu na Mungu;    Ee nuru kutoka mbinguni, an-    gaza moyo wangu huu. 2. Mtoto mpendwa,    nakuomba, chagua moyo    wangu huu, ufanye kuwa hori    lako ukalazwe humo wewe.    Ili nipate mwisho mwema     wa shida yangu na vita.     Zaliwa ndani yangu Yesu,    na ndani yangu ukue. 3. Mwokozi wangu utulize,    tumaini hili kubwa.    Ukija nitakupokea    kwa roho nyenyekevu, hii.    Uweza wangu wote    pia wakungojea kwa     uchu. Nataka     kukutumikia:    Njoo, Yesu usikawie. 

10. Bwana Anakuja

1. Bwana anakuja     twendeni kumlaki,    Bwana Mungu wa     majeshi.    Iwasheni mioyo    tukampokee,    huyo Mwenye utukufu.        /:Karibu Bwana, njoo:/           Shinda pamoja nasi. 2. Wewe ndiwe Mfalme, Mfalme    wa mbinguni,    utulishe wenye njaa.    Wewe ndiwe mwanga,    sisi tu vipofu,    tufanye tuone tena.           /:Karibu Bwana... 3. Wewe ndiwe njia,     tutakufuata,    turudi kwa Baba yetu.     Wewe ndiwe kweli,     utuangazie,    tusije tukapotea.           /:Karibu Bwana...  4. Hosana, Hosana,    huyo mbarikiwa,     anakuja kwetu sisi.    Aja kutulisha    na kutugawia    matunda ya ukombozi.        ...

11. Natoka Leo Mbinguni

1. Natoka leo mbinguni,    naleta habari njema     habari yenye furaha    kwa ninyi na watu wote. 2. Amezaliwa kitoto,    na mwanamwali Maria,    ni mtoto mzuri na mwema,    awaletea furaha. 3. Ni Yesu,    Mwana wa Mungu, Mwokozi    wa ulimwengu,     Atakayekuondoa    makosa yote na shida. 4. Awapa wote wokovu,     uliowekwa na Mungu,     mkae nanyi mbinguni     pamoja nasi milele. 5. Alama yenu iwe hii:     Zizini mtoto maskini     aliyevikwa viguo,    naye ni Bwana wa mbingu. 6. Tumsifuni sisi sote,    tuwafuate wachunga,     tuyaone yale makuu,     tuliyopewa na Mungu. 7. Yesu unipendezaye,     ugeuze moyo wangu,     uwe nyumba yako nzuri,     nisikuache daima. 8. Tumsifu Bwana wa mbingu,    aliyemt...

12. Njooni, Tumheshimu Yesu

1. Njooni, tumheshimu Yesu,    tumtolee sifa zetu.    Tumwimbie kwa furaha,    sisi watu wa Yesu. 2. Baba amemtuma Mwana     atuletee uzima,     utakaopewa watu    wenye shida na kufa. 3. Moyo wake watupenda    kwa upendo amekuja,    aokoe wenye dhambi     wasishindwe na mwovu. 4. Nuru imetutokea,     Yesu akiponda kichwa     cha adui wetu mkali     anayetudanganya. 5. Tutabarikiwa kweli,    tukishika Neno hili,    tukimsifu Bwana Yesu     kwa vinywa na mioyo. 6. Mwana mzuri Bwana Yesu,     twakuomba tupeleke     pale wakuimbiapo     malaika nyimbo nzuri. 

13. Salamu, Yesu Bwanangu

1. Salamu Yesu Bwanangu, Wewe    uzima wangu.     Nimekujia naleta    vyote ulivyonipa:    Ni moyo na mwili wangu, hata    na mawazo yangu,     ndiyo heshima yangu. 2. Umezaliwa Bwanangu     kwa ajili ya mimi;     umenipenda kabisa,    umenipa wokovu.     Tangu  mimi sijaumbwa,     umenitengenezea,     ukombozi wa moyo. 3. Uvuli mzito wa mauti,    ulinifunikiza:      Umenitokea jua,    waniangaza moyo.     Wewe Bwana umenipa nuru,    raha na uzima.     Nakushukuru Bwana. 

14. Siku ya Furaha (Aliyozaliwa Yesu)

1. Siku ya furaha,    siku ya uzima     aliyozaliwa Yesu.           /:Tulipotea Yesu akaja.             Furahini, furahini,               Wakristo! :/ 2. Siku ya furaha,     siku ya uzima     aliyozaliwa Yesu.        /:Yesu ashuka, atuokoe.          Furahini, furahini,          Wakristo! :/ 3. Siku ya furaha,    siku ya uzima     aliyozaliwa Yesu.         /:Malaika wote            wamsifu Mungu.            Furahini, furahini,            Wakristo! :/

15. Tawi Limechipuka

1. Tawi limechipuka    shinani mwa Yese,    kama tulivyopashwa     habari na wazee.    Likatoa ua    wakati wa usiku,     lilipochanua. 2. Isaya alitaja    ua hilo zuri.    Ni Yesu, Mponya wetu,    Maria alimzaa.    Usiku mtulivu.     Uwezo wake Mungu     umefanya hivi.   3. Na ua hili dogo    lanukia vyema;      lang’aa kama jua     giza lafukuzwa.    Ni Mwana wa Mungu     pia mwana Adamu;     Mwokozi wa watu. 4. Siku ya kufa kwetu Yesu    tuongoze, tuiache dunia,    twende furahani    mbinguni kwa Mungu    Pale tutakusifu    Pasipo kukoma. 

16. Tunakuamkia Yesu

1. Tunakuamkia Yesu,     tunakupa pongezi.     Umezaliwa kikiwa,     malaika wakuabudu,     Uwe nasi! 2. Mwana wa Mungu     wa pekee,     Yeye ni  mgeni wetu,    Anajiunga na sisi    Mfalme wa kale na kale!    Uwe nasi! 3. Ashikaye ulimwengu     ashikwa na Maria!    Ni mtoto mdogo na     mchanga!     Tena ni Bwana wa     mbingu! Uwe nasi! 4. Nuru ya milele aja     kuleta mwanga wake.    Aondoa giza lote;    tuwe watoto wa mwanga.     Uwe nasi! 5. Kwetu akawa maskini     kwa kutuhurumia,     tupate mali ya mbingu,    tuwe watoto wa Mungu.    Uwe nasi! 6. Amefanya haya yote     kwa kuwa atupenda.    Kwa hiyo furahini tu     na tumshukuru daima!    ...

17. Tuimbe na Kusifu

1. Tuimbe na kusifu    kwa nyimbo za furaha:    Yesu Bwana wetu     amezaliwa leo    zizini Bethlehemu.    Furaha ya mioyo.    Mponya na Mwokozi,    tunakusifu. 2. Nakutamani sana,     uliyetoka juu.     Ee Mwokozi mwema     tuliza moyo wangu,     unipe neema yako,    Kitoto cha huruma.    Univute juu, univute juu. 3. Rehema zake Mungu     ni nyingi, alimtuma     Mwana wake Yesu,     awakomboe watu,     atufanyie njia,    tufike tena kwetu.     Kwetu ni kwa Mungu,    kwetu kwa Mungu. 4. Na watu wakaao     katika giza wote     wanakungojea    Wewe Mwokozi wetu,     na kukufurahia     uliyetukomboa.    Yesu Bwana wetu twakutukuza.

19. Usiku mtakatifu!

1. Usiku mtakatifu!    Wengine walala     wakeshao ni Yosefu tu    na Maria waliomlinda         Yesu mwana mzuri          Yesu mwana mzuri 2. Usiku mtakatifu!    Wachunga wapewa     habari nzuri na malaika,    zienezwe popote sasa:         Yesu Mponya kaja          Yesu Mponya kaja. 3. Usiku mtakatifu!    Siku ya furaha     imetuangaza Kimungu     tumeupewa ukombozi     Kristo amefika    Kristo amefika. 

18. Umati wa Yesu

1. Umati wa Yesu,    njooni kwa furaha    msikie habari ya sikukuu!    Mwana wa Mungu     azaliwa kwetu.           Njooni tumtukuze!          Njooni tumtukuze!            Njooni tumtukuze!           Yesu Kristo! 2. Mbinguni malaika     wamwimbia wote     na wote wakaao kwake    Mungu.    Mungu ni mkuu,    aliyetupenda.          Njooni tumtukuze! … 3. Tumsifu Mwokozi     Yesu siku zote,     aliyezaliwa kwetu leo.     Anatujia atufurahishe.          Njooni tumtukuze! …

20. Njooni Wachungaji Bethlehemu!

1. Njooni wachungaji     Bethlehemu!     Njooni kumtazama    mtoto mzuri.     Mwana wa Mungu amezaliwa.    Baba amtuma awakomboe.    Msiogope!   2. Twende Bethlehemu tukaone    tulivyoambiwa na malaika.     Tuyaonayo tutatangaza    na kutukuza kwa nyimbo nzuri    Haleluya! 3. Kweli malaika wametangaza    Furaha kubwa kwa wachungaji.     Sasa po pote patengenezwe,     na watu wote watapendezwa.     Furahini!

21. Watoto Njooni Bethlehemu

1. Watoto njooni, Bethlehemu,    njooni zizini kuona makuu    Mungu aliyotutendea leo,    watoto waone furaha kubwa. 2. Twaona kitoto kizuri hapa, wa-    zee wamtazama,    wanafurahi.     Wachungaji wote    wamwangukia,     malaika wa mbingu  wanam-    wimbia. 3. Pigeni magoti na wachungaji!    Wakubwa, wadogo    tumnyenyekee!     Tuimbe na sisi kwa     furaha kuu, nyimbo za     kumsifu Mwokozi Yesu! 4. Watoka mbinguni utuokoe,    waona uchungu sababu yetu,    leo wazaliwa mwana kikiwa.    Halafu wateswa, unatufia. 5. Twapenda kukupa mioyo yetu,    twataka kukutumikia vema.     Takasa mioyo ikupendeze,    tupate kufika kwako    mbinguni.

22. Yesu Kitoto Kizuri

1. Yesu kitoto kizuri,    umetujia watoto     utupe mioyo mizuri,    tuwe watoto wa Mungu. 2. Ee Mwanga toka    mbinguni,     umetufikia sisi,    tupate mwanga wa kweli,    tuunganishwe na Mungu. 3. Mpenzi wangu Mtakatifu,    umezaliwa duniani:      furaha iko kwa wote,    kwa wakubwa na wadogo. 4. Unibariki ni mdogo,     moyo unisafishie,    ondoa taka ya roho,     upendo wetu uzidi! 

23. Msifuni Mungu, Wakristo

1. Msifuni Mungu, Wakristo,    aliyetukuka,    atufungulia mbingu        /:kumtoa mwanawe:/   2. Atokaye kifuani    pa Mungu Babaye,    alala sasa kitoto         /: kitupu, maskini. :/ 3. Anyonya kwa mama yake,    maziwa chakula,    kwa kweli anatulisha         /:chakula cha mbingu.:/ 4. Ageuza hali yake,     avaa mwili wetu     na sisi anatuvika         /: uzima wa Mungu. :/ 5. Akawa mtumwa, na mimi    naitwa kibwana,    niwe nduguye na mtoto        /: wake Mungu Baba :/ 

24. Ulimwenguni Pote

1. Ulimwenguni pote    asifiwe Mungu mkuu     amemtuma Mwokozi,     wakosaji wapone. 2. Zamani wazee wale     wameona hamu kuu,     waondoshwe makosa     na kumpata Mwokozi. 3. Abrahamu, Yakobo    na watu wa Sayuni     walimngojea sana,     sasa ametujia. 4. Karibu Mponya wangu     niondolee woga.    Ujitengenezee    njia moyoni mwangu. 5. Safisha nyumba yako     umfukuze Shetani,     yule nyoka wa kale.    Nikutumikie wee!

25. Mungu ni wa Utukufu

1. Mungu ni wa utukufu     panapo mbinguni juu,     na kwao wampendezao     duniani raha kuu.     Sikieni nchi zote     huko mjini Bethlehemu:         /: Kristo amezaliwa,              Bwana wetu daima. :/ 2. Watu na malaika wote    wanamtukuza Yesu,     ashukaye toka mbingu     kuwa kama maskini.    Akaacha enzi yake,     akavaa unyenyekevu:          /: Kristo amezaliwa,.. :/ 3. Asifiwe Mungu Mwana     na Mwokozi wa watu,     mleta mwanga na uzima     Yesu mshinda kuzimu, Mfalme    wa utengemano     huko mjini Bethlehemu.        /:Kristo amezaliwa, ...:/ 

26. Nchi, Mbingu Furaha!

1. Nchi, mbingu furahi!    Haleluya!    Amekuja Mwokozi,     Haleluya!           Mwana wake Mungu           amekuja kwetu,           Mwana amekuja kwetu. 2. Toka shina la Yese,    Haleluya!    Tawi limechipuka,     Haleluya!         Mwana wake Mungu… 3. Neno lake Mwenyezi,     Haleluya!     Limekuja duniani,     Haleluya!         Mwana wake Mungu …

27. Amezaliwa Mtoto

1. Amezaliwa mtoto     mjini Bethlehemu.    Nimemchagua yeye,     niwe mali yake!     Oye, oye, niwe mali yake! 2. Nataka kuingia     pendoni mwake yee    na kumtolea moyo     hata vyangu vyote,    Oye, oye, hata vyangu vyote. 3. Kwa moyo wote safi     nataka kumpenda     shidani, furahani    hata kila wasaa.     Oye, oye, hata kila wasaa. 4. Unikubali hivyo,    naomba kabisa    nikuishie Wewe,     leo na daima!    Oye, oye, leo na daima!

28. Amkeni Upesi

1. Amkeni upesi wachunga     kondoo!     Malaika washuka,    habari watupa:         Furaha karibu,         Mwokozi aja! 2. Wachungaji njooni,    tumtafuteni!    Akiwa zizini pigeni filimbi.          Furaha karibu … 3. Wachungaji hima washika njia.    Pamoja wamwona     mamaye, babaye.          Furaha karibu … 4. Wamjua upesi mtoto wa     mbingu.     Wapiga magoti      kumwimbia nyimbo.           Furaha karibu … 

29. Siku ya Furaha Popote

1. Siku ya furaha popote,    Sauti za kusifu zavuma!     Duniani, nyumbani     nyimbo za furaha kuu:     Siku ya furaha popote,    Sauti za kusifu zavuma!    Wote na tushiriki     furaha yetu,    mwanga wa ulimwengu     waja toka juu.         Siku ya furaha popote,         Sauti za kusifu zavuma!          Duniani, nyumbani          nyimbo za furaha kuu:         Siku ya furaha popote,          sauti za kusifu zavuma!  2. Siku ya furaha popote,      Sauti za kusifu zavuma!      Duniani, nyumbani,      nyimbo za furaha kuu:     Siku ya furaha popote,      Sauti za kusifu zavuma!      Azaliwa Mesiya kwetu      duniani:      ...

30. Mpige Mbio, Wachungaji

1. Mpige mbio, wachungaji      mpige mbio wote,     Chukueni na filimbi na     zumari pia.    Mpige mbio wote,    mpige mbio wote     Bethlehemu kwenye hori    walishwamo ng’ombe. 2. Mumtazame mtoto mzuri    aliyezaliwa,    na wazazi wake mtoto     wako huko naye.    Ni Yosefu baba     na Maria mama,    mwanamwali mzuri sana    kama malaika juu. 3. Hebu njooni, ee jamani     mlete nguo nzuri!    Tumlazeni mtoto wetu    kwa uzuri wote!     Twakubembeleza     wewe mtoto lala!     Lala Yesu mpenzi wetu     twakubembeleza.

31. Malaika Njooni Toka juu!

1. Malaika njooni toka juu!    Oye, oye, tazama,    tazama kitoto.    Imbeni, pigeni panda.     Haleluya! Haleluya!     Nyimbo za Yesu na Maria! 2. Kwa sauti kuu mwimbieni!    Oye, oye, tazama,     tazama kitoto.    Kwa vinanda na vinubi.     Haleluya! Haleluya!     Nyimbo za Yesu na Maria!   3. Tungeni nyimbo tamu mno,    Oye, oye, tazama,    tazama kitoto,    kupita ndege wa anga.     Haleluya! Haleluya!     Nyimbo za Yesu na Maria! 4. Utamu wa nyimbo zenu,     Oye, Oye, tazama,      tazama kitoto.     Umbembeleze, alale.     Haleluya! Haleluya!     Nyimbo za Yesu na Maria!   5. Watu na watengemane,     Oye, oye, tazama,     tazama kitoto.    Na Mungu tumpe    ...

32. Kitoto Mpenzi Lala Wee

1. Kitoto mpenzi lala wee,    Kitoto wa mbingu!    Malaika wakupepea     ulale kwa raha.     Nasi maskini wachunga     tunakubembeleza wee.     Lala, ulale: Kitoto wee, ulale. 2. Maria kwa upendo mkuu      amlaza vizuri.    Yosefu amekaa kimya     ili asimwamshe.    Na wanyama wa nyumbani     wamenyamaza kabisa:     Lala, ulale: Kitoto wee, ulale. 3. Yesu utakapokua,    watakuumiza.     Kilimani pa Golgota,     utasulibishwa.    Kwa hiyo sasa lala tu!     Kwa raha na utulivu!     Lala, ulale: Kitoto wee, ulale.

33. Niende na Wachungaji

1. Niende na wachungaji     nimtazame Mponya wangu,    kazaliwa duniani    kwa kunipenda mimi. 2. Nimwimbie na malaika,     niusifu utukufu.     Anautengemaza,     kila moyo umpende. 3. Nikawaze na Maria     jambo hili la ajabu:    Aacha mwili mzuri,     achukua wa kimtu. 4. Nimpelekee vipaji     na watambuzi wa nyota,     na nimpe mali yangu,     hata uzima nimpe. 5. Nakupenda, u Mwokozi,    nikumbuke siku hii.    Uje mwangu moyoni,     uufanye kikao. 

34. Wakristo Furahini

1. Wakristo furahini,    furahini sana!     Mwaipigiwa leo     mbiu yenu njema!     Malaika wanaimba     huko juu mbinguni,    /: wanaimba vizuri     sauti ya kushangaa! :/ 2. Hivi wanavyoimba:     Furahini nyote!     Acheni kuogopa,     tazameni nyote    kwani amezaliwa     Mwokozi wa pekee:    /: ni Bwana Yesu Kristo,     Mwana Mungu wetu:/ 3. Shangilieni nyote     na  kusikiliza.     Wapigieni nyote     mbiu na sauti kuu.     Mungu katupa sote     mtoto wa mbinguni,    /: kwa kutupenda sisi     amekuja kwetu. :/

35. Tazama, Nawatangazia

Tazama, nawatangazia, nawatangazia, nawatangazia,  shangwe kubwa,  shangwe kubwa,  shangwe kubwa,  shangwe kubwa. Shangwe,  shangwe kubwa inayokuja,  kwa watu wote, wa koo zote; inayokuja, inayokuja. Amezaliwa leo,  Bwana Mwokozi,  ndiye Kristo Yesu,  Bwana wa mjini!  mwa Daudi,  Bwana wa mjini  mwa Daudi,  wa mjini mwa Daudi! 

36. Mwema, Mwema,Mwema

Mwema, mwema, mwema ni Bwana mbinguni,  na utengemano  kwa watu wanaompendeza,  kwa watu wanaompendeza.  Mwema ni Bwana mbinguni.  Mwema ni Bwana mbinguni,  nchi itengemane, watu wapendezwe,  wote wakampendeze Bwana.  Mwema, mwema,  mwema ni Bwana mbinguni  na utengemano  kwa watu wanaompendeza  kwa watu wanaompendeza!

37. Sote Tufurahi

1. K: Sote tufurahi,     W: habari ni njema     K: Njooni nyote wahi,      W: tupate uzima           Sasa yametimia            yaliyotabiriwa            Mwokozi kazaliwa.   2. K: Kule Bethlehemu      W: Yesu kazaliwa      K: Mama Mariamu      W: alivyoambiwa. Sasa …   3. K: Kumbe, huyo Mwana     W: kalazwa horini     K: Huyo Yesu Mwana    W: akawa shidani.  Sasa … 4. K: Mwana atiiye     W: ni Bwana shujaa,      K: Kwake tuwe wana,      W: ni Mponya dunia.  Sasa …  5. K: Jeshi la mbinguni     W: katoa Injili.     K: Watu malishoni,     W: kaona ni kweli.  Sasa … 6. K: Mungu yupo nasi     W: katika dunia. ...

38. Sauti Imetoka Mbinguni

1. K: /: Sauti imetoka mbinguni;     W:    Sauti imetoka mbinguni. :/     K: /: Ahubiri malaika            wake Mungu;     W:    Ahubiri malaika            wake Mungu:/   2. K: /: Ninyi watu acha kuogopa;    W:    Ninyi watu acha kuogopa:/     K: /: Nawaletea habari,            furahini;     W:    Nawaletea habari,            furahini:/   3. K: /: Leo amezaliwa Mwokozi;     W:    Leo amezaliwa Mwokozi:/     K: /: Kazaliwa Kristo ni           Mwokozi wenu:/      W:    Kazaliwa Kristo ni            Mwokozi wenu:/   4. K: /: Mtamwona            kal...

39. Tumezaliwa Mtoto

1. K:  Tumezaliwa mtoto,         tumezaliwa mtoto.          Ni Bwana Yesu,          Mwana wa Mungu         Atakayewachunga          kondoo.    W:  Amezaliwa mtoto.         Asante, Bwana Mungu.        /: Ulivyoona kondoo wako,          huku chini ya mbingu,          hawana Mchungaji. :/ 2.  K:  Wewe Mama Mariamu,          wewe Mama Mariamu,          Utaziona huzuni nyingi          atakapotimiza sheria.     W:  Wewe Mama Mariamu,           na umshukuru Mungu,         /: Alivyoona kondoo wake,          huku chini ya mbingu,          hawana Mch...

40. Tushangilie Sote

K:  Tushangilie sote  W:  Kila mtu.  K:  Mwana wa Mungu        akaja W:  Hata kwetu.  K:  Tumjue Mungu Baba  W:  Wa huruma.  K:  Usiku wa manane  W:  Shangwe kubwa  K:  Alipozaliwa Kristo  W:  Awe Mfalme.  K:  Pale katika mji  W:  Wa Daudi.  K:  Kwenye kondoo hata        ng’ombe W:  Bethlehemu.  K:  Na akaitwa kwa Jina W:  La ajabu.  K:  Nalo Yesu Mwokozi  W:  Mungu nasi.  K:  Hakika ni Mwokozi  W:  Mwenye enzi K:  Tupatiwe uzima W:  Wa milele.  K:  Na kumtumikia daima  W:  Siku zote.  K:  Maana kwake        sasa tumemwona  W:  Mungu wetu.  K:  Na hivyo hata Roho  W:  Mtakatifu  K:  Njoni kwa hiyo       tumsifu W:  Bila mwisho.

41. Tumepata Mwokozi

1. K: Tumepata Mwokozi sasa     W: Bwana Yesu    K: Ee, ee!     W: Tumepata Mwokozi sasa. 2. K: Duniani hatuna mtu    W: Hata mmoja     K: Ee, ee!     W: Duniani hatuna mtu. 3. K: Tutafute msaada wapi     W: Huku chini     K: Ee, ee!    W: Tutafute msaada wapi?   4. K: Peke yetu tungepotea.     W: Peke yetu.     K: Ee, ee!    W: Peke yetu tungepokea 5. K: Yuko Yesu peke yake tu,    W: Yuko Yesu.     K: Ee, ee!    W: Yuko Yesu peke yake tu.   6. K: Asema, Nakufia wewe     W: Mwanadamu,     K: Ee, ee!     W: Asema, Nakufia wewe.   7. K: Katumwagia damu yake     W: Msalabani.      K: Ee, ee!     W: Katumwagia damu yake.   8. K: Katulipia dhambi sisi     W: Wakosaji....

42. Ilitoka Nuru Kuu

1. Ilitoka nuru kuu,     kuliko nuru zote.     Na huo wimbo wa juu     wapita nyimbo zote;     Ndiyo habari tukufu,     ya Kristo wa utukufu,     awajia wapole;    Ni Mungu pamoja na sisi,    Imanueli. 2. Mwaka huandama mwaka,    wimbo huu na uimbwe;    Wapenda kukumbusha,     mzee na wanawe,     ndiyo habari tukufu,    ya Kristo wa utukufu,      awajia wapole;     Ni Mungu pamoja na sisi,    Imanueli 3. Twafurahi siku hii      ijavyo kila mwaka;     Nasi tufanye bidii     huku tukikumbuka,     Ndiyo habari tukufu,     ya Kristo wa utukufu,     awajia wapole;    Ni Mungu pamoja na sisi,    Imanueli.

43. Yesu Ulale

1.  K:  Yesu, ulale,     W:  Haleluya      K:  Yesu, ulale,      W:  Haleluya      K:  Tulia, Mwana,       W:  Haleluya     K:  Tulia, Mwana,      W:  Haleluya     K:  Mwana wa Maria,      W:  Haleluya      K:  Mwana wa Daudi,      W:  Haleluya      K:  Shina la Yese,      W:  Haleluya      K:  Haleluya,      W:  Haleluya          Mtoto, Ee,           mwema tu,          Kila anayekuamini,            Utamgawia amani tu. 2.  K:  Lala, Ee Yesu,       W:  Haleluya      K:  Lala, Ee Yesu,      W:  Haleluya  ...

44. Mjini Mwake Daudi

1. Mjini mwake Daudi     bandani mwa mifugo     mtoto alizaliwa     na mamaye maskini    Mariamu ni mama    Yesu mwanawe mwema. 2. Yesu akawa mbinguni     akatoka enzini     hakukaribishwa chini     akalazwa horini     akaja kimaskini    kuketi duniani. 3. Siku za ujana wake     akimheshimu mama      na kumtii katika yote     kama alivyosema.     Kila mwana na awe     mtii kama Yeye. 4. Amekuwa hata sasa     kielelezo chetu     alikuwa na unyonge     kama unyonge wetu     kucheka na kulia    ni kama sisi sote. 5. Tutamwona waziwazi     ndiyo ahadi yake     sasa aketi mbinguni     katika enzi yake    sote na tumwandame     kwani ni Mfalme ...

45. Bwana Yesu Amezaliwa

1. K: Bwana Yesu,    W: Ee, amezaliwa.     K: Wachungaji,    W: Ee, wamsujudia.     K: Na mamajusi,    W: Ee, wamsujudia.     K:/:Na sisi sote,    W: Ee, tumsujudie. :/ 2. K: Amefika,    W: Ee, atukomboe.     K: Atimize,    W: Ee, ahadi ya kale.     K:  Aliahidi,    W: Ee, Yeye peke yake    K:/:Na sisi sote    W: Ee, tumsujudie. :/ 3. K: Isaya naye,    W: Ee, alitangaza.     K: Kwamba Mwokozi,     W: Ee, atazaliwa.     K: Tangazo lake,     W: Ee, limetimia.      K:/:Na sisi sote,    W: Ee, tumsujudie. :/ 4. K: Malaika,    W: Ee, waona furaha.     K: Wamwabudu,    W: Ee, na kumwimbia.     K: Na nyimbo zao,    W: Ee, zimesikiwa.     K:/:Na sisi sote,...

46. Twendeni Tumshukuru

1. Twendeni tumshukuru     na kumwimbia Mungu,    aliyetupa roho     na nguvu mpaka leo. 2. Twaenda na kukua     miaka yetu yote.    Hivyo mwaka kwa mwaka    twafikia uzee. 3. Twaona shida nyingi,     uchungu na mateso     na vita na misiba     katika ulimwengu. 4. Kuhangaika kwetu     siku zote ni bure     asipotushikiza     Yeye atulindaye. 5. Na kama mama mwema ana    vyomlinda mtoto     katika shida zote,     asipotee njia. 6. Hivyo na Mungu wetu     hulinda watu wake,     huwakingia shida,     huzuni na misiba. 7. Leo atuingiza     katika mwaka mpya,     hachoki kutupenda,    kutufanyia mema. 8. Huruma zako ni mpya     kila panapokucha,    hizo zinakomesha    ...

47. Anza Siku Yako Hii

1. Anza siku yako hii kwa Jina la Yesu;     Mwombe akujalie, usimame naye.    Kazi zako zote wee atazibariki.    Na tena ulalapo, atakuwa kwako. 2. Asubuhi mapema     umwombe Mwokozi,     akusaidie Yee shidani popote.    Atasimama kwako siku kuchwa pia,     na kumshinda Shetani akikujaribu. 3. Yesu akiwa nawe, waacha maadui,     usiogope hila zao zote mbaya.     Umtegemee Yesu,     shika mkono wake;     mtegemee Mwokozi,     Yeye atashinda. 4. Mambo yangu na shida    ninakuwekea    kama unavyopenda, zimalize zote.    Kazi yangu nianze kwa Jina la Yesu     nakuomba: njoo kwangu,     unisaidie!

48. Yesu Mponya tu Hapa

1. Yesu Mponya tu hapa,     moyo watulia,    mawazo yetu yote    uyavute kwako.    Mwanga wa Neno lako,     utuangaze wote,    tuwe na mwangazo. 2. Kaa karibu nasi, tunakutamani,    mfunzi wetu ni wewe,     sisi wanafunzi.     Nenolo lina nguvu,     litatufanya wapya, laongoza vema. 3. Tuna furaha kubwa, tunakungojea.    Wewe u mwamba wetu     tutegemeao. Bwana tunakushika    mpaka tunapofika uzimani kwako. 4. Twataka utufunze kuwa na upole.     Tufanane na wewe unyenyekeavyo.     Utimizavyo kazi, ulivyofanya bidii     kuwa mpatanishi. 5. Nguvu ya Roho wako     ionyeshe kwetu,     unavyomulikia wanaopotea.    Kwa kinywa chako Yesu     utushindie nasi,     tuwe wako kweli!

49. Nakutegemea Yesu

1. Nakutegemea Yesu,    Yesu peke yako tu.     Wewe u Mkombozi wangu    unitulizaye.     Nakutegemea Yesu,    kwani u Mkombozi ukinifia.    Ndipo nikakupenda sana,    wala sikuachi! 2. Wewe mfalme mkubwa sana    unaondoa dhambi.     Wanionea huruma,     huna madanganyo.          Nakutegemea Yesu, … 3. Wewe umechunga kondoo,    ukitanguliza mwanga.    Nakungoja mwongozaji,     nisipotee njia.           Nakutegemea Yesu, … 4. Wanichukulia mzigo,     sianguki majini.     Natambua wanipenda,     huniachi pekee.          Nakutegemea Yesu, … 5. Bwanangu umeniweka    ufalmeni ni kuzuri.     Naisifu damu yako     inayoniosha.          Nakutegemea Yesu, …

50. Twapenda Ukaapo

1. Twapenda ukaapo     Bwana wetu enzini,    furaha zako wewe     zinazipita zote. 2. Palipo pa kuomba     wajapo watu wako     na wewe Bwana upo,     uwakubali wote. 3. Twapenda Neno lako,     habari za wokovu,    za nguvu za kushinda,    za shangwe za mbinguni. 4. Twapenda nyimbo zako,     tunaziimba hapa,    mpaka tutaziimba     pamoja na malaika. 5. Utujalie Yesu,     tuzidi kukupenda,     tuone uso wako     utakavyotakata. 

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu

1. Yesu ndiye kiongozi wangu,    kumfuata Yeye ni furaha,     ajuaye kuongoza vema,     anilinda, nisione shida,    analeta raha moyoni. 2. Bwana Yesu akiniongoza,     nitapita pori na misitu,     nitavuka mito na bahari     kwa furaha, kwani nina njia    ya kufika mjini kwa    Mungu. 3. Nikilala Yesu anilinda,     anitunza Yeye siku zote. Hata     nikifika njia panda, nikiona    shaka, aonyesha     njia ya kufikia kwake. 4. Siku zote namfuata Yeye,    sitaona kiu wala njaa;     anitunza kwa rehema nyingi:    nitaweka mikononi mwake    moyo wangu, auokoe. 

52. Jina Lake Yesu Tamu

1. Jina lake Yesu tamu;     Tukilisikia.     Hutupoza, tena hamu     hutuondolea. 2. Roho iliyoumia     kwalo hutibika,     chakula njaani pia;     raha, tukichoka. 3. Jina hili ni msingi,    ngao, ngome, mwamba,     kwa hili napata wingi    kwangu ni akiba. 4. Yesu, Mchunga, Rafiki,    Mwalimu, Kuhani,     Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,    Uzima kifoni. 5. Moyo wangu hauwezi    kukusifu kweli,     Ila sifa zangu hizi,    Bwana zikubali. 6. Na utakaponiita,     kuja kwako Bwana,     huko kwako sitaacha     kukusifu sana.

53. Tumshukuru, Tumsifu

1. K: Tumshukuru, tumsifu        Mungu kwani ni mwema.    W: Huruma yake ipo,        Mchana na usiku. 2. K: Tangaza Jina lake,        Mungu wetu wa kweli.    W: Huruma yake … 3. K: Kajaza maajabu,        Mbinguni duniani.     W:  Huruma yake .. 4. K: Kwa uwezo wake mkuu,       ameviumba vyote.    W: Huruma yake .. 5. K: Aliongoza watu,        ugenini zamani    W: Huruma yake .. 6. K:  Maskani ametupa,         hapa ulimwenguni.     W:  Huruma yake .. 7. K: Anawalisha watu,        hata wanyama pia.    W: Huruma yake .. 8. K: Na tumwimbie Mungu,        kwani Yeye ni mwema.    W: Huruma yake ..

54. Yesu, u Nyota Kubwa

1. Yesu, u nyota kubwa,     itokayo kwa Yakobo,     moyo wangu wapenda     kukutumikia leo.     Ukubali vipaji     niviletavyo mimi. 2. Ninaleta dhahabu,     ndio kukutegemea,    nalo ni paji lako,     ulilonipa mwenyewe;    nikushike kwa kweli  hata    majaribuni. 3. Nao uvumba wangu    ni maombi yangu mimi;     midomo na mioyo     isikome kuyatoa.    Uyakubali haya    kuwa uvumba mzuri. 4. Nayo majuto yangu     ndiyo manemane yako;     kwani hunipokea,     nikikujutia kweli.     Nasema kwa furaha:    Watwaa matunzo yangu! 

55. Mmoja Ndiye

1. Mmoja ndiye tumpendaye,    aliyetoa mwili wake     akikubali mateso.    Twakupa mioyo yetu     Mwokozi uliyetufia,     twapenda kuwa wako tu.     Bwana tukubali! Ututengeneze     sisi wako. Nuru yako itung’aze     tusipotee gizani. 2. Sisi hatukukuita,    ila umetuita wewe,    huruma yako ni kubwa.     Nguvu zetu hazitoshi,     kukufanyia kazi njema     usipotutia nguvu.    Shida yetu sisi ndio ulegevu,    uondoe; nia zetu zigeuzwe     tufanye kazi kwa bidii. 3. Yesu, wewe umesema:     “Watenda kazi ni wachache      kwenye mavuno ya Bwana.”     Twaomba: Tutume nasi,      tualike wageni wengi,      nyumba ya Bwana ijae.     Heri watu wale uliochagua      kuja kwako kwenye raha   ...

56. Mmoja ni Mfalme

1.`Mmoja ni Mfalme     shujaa, ni mshindaji!    Enyi adui, kimbieni tu!    Nawe Sayuni uone furaha    ukapumzishe kabisa moyo:    Uzima, utengemano, furaha    ndizo Mwokozi atakazokupa. 2. Twende kuonja maji ya uzima     tunayopewa na Bwana Yesu,     aliyesema     “Njooni kwangu nyote,      nitapumzisha mioyo yenu.”     Nyweni, wapenzi, katika kisima     chenye wokovu      wa wenye huzuni. 3. Mfalme wa mbingu     ataka kuwapa     kilemba kizuri cha urembo,     awawekea vitu vya milele,    heshima hiyo ni ya kushinda.    Vumilieni taabu na shida:     Yesu mwenyewe ni tuzo la vita. 4. Nguvu, ujuzi, heshima na sifa     ni zake Mungu     na Mwana wake.     Nami nataka kufika mbinguni!     Nifungu...

57. Nani Mpenzi Wangu Mkuu?

1. Nani mpenzi wangu mkuu?    Nani ninayemsifu?     Nani ninayemjua?     Nani ninayempenda?        /:Ndiye Yesu Mwokozi.:/ 2. Nani nimtegemee,     anipaye moyo mkuu?     Nani aondoaye,     makosa, shida zangu?           /:Ndiye Yesu Mwokozi.:/ 3. Nani anayenipa,    nguvu nyingi za roho?     Nani anifanyaye,    mwenye haki kwa Mungu?         /:Ndiye Yesu Mwokozi.:/ 4. Nani mwenye faraja,     nikiona huzuni?    Nani atulizaye,     moyo wenye taabu?        /:Ndiye Yesu Mwokozi.:/ 5. Nani azishindaye,     hata nguvu za kufa?     Nani anipeleke,    baadaye kwake Mungu?           /:Ndiye Yesu Mwokozi.:/

58. Jina Moja ni Kubwa sana

1. Jina moja ni kubwa sana:    Ni Jina lako Bwanangu! Nasifu    Jina hili lako,     Yesu Kristo u Mwokozi.    Li tamu kwangu Jina hili,    jina jingine silijui. 2. Naliandika Jina hili     rohoni mwangu kabisa.     Silisahau siku zote,     halifutiki moyoni.    Li tamu kwangu Jina hili, jina     jingine sitafuti. 3. Jina hili ni jua langu     lawaka ndani ya roho.    Lanipa na utengemano,    lafuta makosa yote.    Li tamu kwangu Jina hili, jina    jingine sifahamu.      baadaye kwake Mungu? 4. Jina hili ni boma langu,     upanga wangu vitani,    ni ngao yangu na silaha,     lamshinda hata Shetani.    Li tamu kwangu Jina hili, jina    jingine silitaki. 5. Jina hili lanipa nguvu, niweze    kwenda kwa haki. Ujuzi wote  ...

59. Kazi ni Yako Bwanangu

1. Kazi ni yako Bwanangu     tunayoifanya;    hakuna anayeweza     kuvunja kazi hii.    Ni kama punje ya mbegu     ikiwa ndani ya mchanga,    inakufa kwa kuoza;    na hapo yabadilika,     inaota, yakua na kuzaa. 2. Yesu, umeteswa kwanza,    halafu umepaa.    Nao wakufuatao     wanateswa vivyo.    Twaomba tusaidie     nasi tushike njia hii,    kwa kufa kwako na sisi     tunatoka kaburini.     Tuongoze, tufike mbinguni. 3. Bwana wewe umekufa     kwa ajili yetu.    Ukaweka ufufuo      ulipofufuka.    Twaomba: Tuma mitume,    wajulishe Jina lako    mpaka mwisho wa dunia.     Utukubali na sisi    kwa kazi hii, tutume,    twakutii!

60. Ufalme wa Mungu

1. Ufalme wa Mungu     uenee popote!      Nguvu yako iokoe      wakaao gizani.     Uondoe woga wote,    ukawape watu uzima,    ufalme wa Mungu. 2. Ushinde upesi!    Uharibu ufalme    wa Shetani duniani,     ndiye mfalme wa giza.     Nawe utamshinda yeye,     kwani una nguvu ya Mungu.    Ushinde upesi!! 3. U Shujaa wa Mungu!    Kwa rehema ya Bwana     urudishe watu kwako,     wapendane kwa moyo,     wawe raia wako pote.    Ndipo utatukuzwa sana!    U shujaa wa Mungu! 4. Duniani popote     Jina lako livume     nguvu zako zisifiwe     na makabila yote,    uliowatengemaza,     mpaka utakapotawala     duniani popote! 5. Shikeni amri hii:    Tangazeni popote ...

61. Sifuni Nyote Huruma

1. Sifuni nyote huruma ya    Mungu,     kwa nyimbo nzuri,     umati wa Yesu!     Atualika furahani:    /: Msifuni Bwana kwa       neema yake! :/ 2. Yeye ni Mfalme     anayetawala;     viumbe vyote     vinamtumikia,     hata malaika     wamwabudu,   /: wanamwimbia kwa      sauti nzuri. :/ 3. Enyi mataifa, hofu     iacheni!    Njooni kwa Yesu,    Mchunga kondoo     mwema.    Sikilizeni Neno lake:    /: Atukomboa kwa kufa      kwake.:/ 4. Awapa watu chakula     chochote,    atushibisha kama baba    mzuri,    aleta jua hata mvua,    /: atubariki kwa wema      wake. :/ 5. Sifuni nyote huruma ya    Mungu,    kwa nyimbo nzuri,    ...

62. Uamke Kwetu Tena Roho

1. Uamke kwetu tena Roho wa     mashahidi wale wa kwanza,    waliokesha siku zote,     waliomshinda yule adui,     wakihubiri Neno la Yesu     kwa watu wa ulimwengu wote. 2. Uwashe moto wa upendo,    uendelee pote kuwaka.     Peleka watu mavunoni,    wanaofanya kazi kwa bidii.    Bwana mwenye mavuno,     tazama:     Watenda kazi yako ni haba. 3. Mwanao ametuagiza kuomba    hivi kwa Jina lake,     na sisi wanafunzi wake,    twashika Neno lake kwa bidii.     Twaomba hivi kwa moyo wote.    Ee Bwana usikie, ufanye! 4. Utume watu wengi sana,    walitangaze Neno kwa nguvu.    Tusaidie, tuokoe;     ufalme wa Shetani uishe.    Usimamishe, Bwana wa    mbingu,    ufalme wako     ulimwenguni! 5. Utume mwema na uende ...

63. Yesu Mfalme Utiishe

Yesu, mfalme, utiishe upesi ulimwengu wote, viumbe vyote vikutii.  Ubariki Neno lako, utoe Roho wa uzima, uamshe wanaolala. Bwana, usikie  tunavyokuomba.  Amen, Amen!  Tutaimba Haleluya  na nyimbo za kukusifu.

64. Yesu Mwokozi

1. Yesu Mwokozi     mwenye nguvu zote,     wewe Mwana wa Mungu      nitakupenda, nitakusifu, uliye    mpenzi wangu mkuu. 2. Uzuri wote     wa nchi na milima     unatufurahisha.     Yesu ni mzuri kupita hiyo     anatufariji sisi. 3. Jua na mwezi     hata nyota zote     zinang’aa  mbinguni.     Yesu ashinda uzuri huo,     ang’aza watu mioyo. 4. Uzuri wote    hapa na mbinguni    ni mfano wa Mwokozi.    Tumpende Yeye wa utukufu     aliyetupenda kwanza.

65. Yesu ni Mponya

1. Yesu ni Mponya, aleta furaha!     Mwanzo na mwisho     wa vyote ndiye.     Mwana Adamu     na Mungu wa kweli    ametujia atubariki.    Mbingu, dunia, toeni habari:     Yesu ni Mponya, aleta furaha! 2. Yesu ni Mponya, aleta wokovu!    Sikilizeni habari njema!    Sisi tulipomwacha Mungu wetu     akaturudisha tena kwake.     Ametufanya watoto wa Mungu.    Yesu ni Mponya, aleta wokovu. 3. Yesu ni Mponya, aleta uzima!     Kamba za kufa zimekatika.     Mwana wa Mungu      kumshinda Shetani,     awakomboe watumwa wake,    amewapata, kawapa uhuru.    Yesu ni Mponya, aleta uzima. 4. Yesu ni Mponya,     Mchungaji wa kweli,     anayelisha vizuri kondoo.     Wote walio mbali awaita,     awarudishe kun...

66. Mfalme ni Yesu Pekee

1. Mfalme ni Yesu pekee,    wote wanamwangukia,     watawalishwa na Mungu,    Ndimi zote ziungame     Yesu ni Mfalme wa pekee,    atukuzwe popote. 2. Mfalme mkubwa, watu wako     wakutii, wanakusifu.     Yesu apita wafalme,    Yeye ndiye mkubwa sana,    apenda kuwakomboa,     kwani ndiye Mwokozi.   3. Enyi watu mpeni mioyo,    mnaohuzunika njooni;     wakiwa semeni naye,     kwani vyote aviweza.    Awagawia uzima     wanaomngoja yeye. 4. Kama wataka uzima,    nenda kwake, acha soni,    Yeye anakungojea.    Amejitoa mwenyewe,     wewe upate kurithi,    mbingu ni yako sasa. 5. Nimsifuje Yesu Kristo     mimi vumbi, mimi jivu?     Nasema: Nitamtangaza     Kristo Yesu ndiye Bwana!     Na...

67. Nyesha Mvua

1. Nyesha mvua, nyesha mvua,    wewe Roho wa Baba,    nchi kavu ikanyweshwe,     imsifu Mungu wetu! 2. Vuma sana, vuma sana     Roho mwenye uzima,     tulio na usingizi    utuamshe kwa mkono! 3. Toa mwanga, toa mwanga,    Roho kwani unang’aa    wewe ushinde usiku     tusikae na giza. 4. Sikiliza, sikiliza,    wewe Mfalme wa mbingu!    Tuma Roho wako kwetu,     kote kuwe na upya! 

68. Nitakutukuza

1. Nitakutukuza, nakuimbia    /: wewe uzima wangu,     kingojeo changu! :/ 2. Umeniokoa kwa mkono wako,    /: nalifuata njia     ya upotevuni. :/ 3. Wote wakujue upole wako,   /: wakufuate Yesu     ninayekupenda. :/ 4. Utume mitume waende kote,    /: kwa nguvu yako Bwana wafu     wafufuke. :/ 5. Huku chini kote, dunia nzima    /: lifanywe kundi moja, wewe    Mchunga wao! :/ 

69. Wito Waja

1. Wito waja, kwa nchi zote wapi    washindi wa Yesu     watakaomfuata kweli?     Sisi tujitie kwake!     Mkubwa nani?    Tushikane     naye mfalme, tupatane,    tumfuate! 2. Ana ufalme tangu kale,    nchi hata mbingu ni zake.     Atuelekeza juu kwake,     hatahukumiwa tena.     Mkubwa nani? …  3. Tutangaze utume mwema kwa    makabila ya kwetu, na tuseme     pasipo woga tuyaonayo kwa    Yesu.        Mkubwa nani? …  4. Haya jamaa tuwe tayari      sisi watumishi wake,     Yeye ni Mfalme wa    majeshi,     miili na mioyo ni yake.         Mkubwa nani? … 

70. Twende Vitani

1. Twende vitani vitakatifu,     zikitujia, shida na taabu.     Ngurumo zivume kutia woga.    Mwiteni Mwokozi!     Yesu ni mwanga. 2. Ingawa giza lawafunika,     na raha yenu ikizimika,    na nguvu za mwovu     hazina mpaka.          Mwiteni Mwokozi … 3. Shetani aje, akijaribu     kuvunja kazi na kuharibu     hila zake zote na zitakwisha.          Mwiteni Mwokozi … 

71. Wajibu Mwema Watoka Kwako

1.  K:  Wajibu mwema          watoka kwako,           Bwana mwenye           utukufu.         Neno jema ndilo           Jina lako.     W: /: Yesu ni mwanzo          wa kazi shambani,           tena ni Bwana,          wa nguvu kwa utume          wetu.:/ 2.  K:  Watendakazi mwako           shambani,          uwape matumaini.          Nazo nguvu wakiwa           kazini.     W:  /: Watende yote kwa          uaminifu,          wawe makini,          huduma isiharibike. :/ 3.  K:  Wapate heri        ...

72. Tumesikia Mbiu

1. Tumesikia mbiu:     Yesu, loo! Aponya;     itangazeni kote,     Yesu loo! Aponya.     Tiini amri hiyo:      nchini na baharini,     enezeni mbiu hii:     Yesu loo! Aponya. 2. Imbeni na vitani:     Yesu loo! Aponya;     kwa nguvu ya Mkombozi,     Yesu, loo! Aponya.    Imbeni wenye shida,     Unapoumwa moyo,     na kaburini imba:     Yesu, loo! Aponya. 3. Mawimbini ienee:    Yesu, loo! Aponya:     wenye dhambi jueni:     Yesu, loo! Aponya     Visiwa na viimbe,     vilindi itikeni,     nchi  shangilieni:     Yesu, loo! Aponya. 4. Upepo utangaze:     Yesu, loo! Aponya;    mataifa yashangaa;     Yesu, loo! Aponya.     Miliman...

73. Ni Ujumbe wa Bwana

1. Ni ujumbe wa Bwana Haleluya!    Wa maisha ya daima.     Amenena mwenyewe, Haleluya!    Utaishi ukitutazama.     Tazama! Ishi sasa!     Kumtazama Yesu.       Amesema mwenyewe,      Haleluya!     Utaishi ukitazama. 2. Ni ujumbe wa wema,  Haleluya!    Nawe shika, rafiki yangu.     Ni habari ya raha, Haleluya!    Mwenye kuisema ni Mungu.         Tazama … 3. Uzima wa daima, Haleluya!    Kwake Yesu utauona.     Ukimtazama tu, Haleluya!    Wokovu pekee wa Bwana.          Tazama …

74. Bwana Uliyewaita Watakatifu

1. Bwana uliyewaita,     watakatifu wako,    wawe mitume, wachunga,    walishe kundi lako;     Wanyonge na wenye hofu    wakawa mashujaa,     na wapole wa kunena    wasiwe kunyamaa. 2. Hata leo wawataka     watakatifu wako,     nawe wauliza tena,    ni nani aliyeko atakaye     nimtume afundishe vijana?    Ni tayari, Bwana wangu,     Nitume mimi Bwana. 3. Nitume na mimi, Bwana,     kama ulivyotumwa,     habari ya msamaha,     na dhambi kutubiwa,     niwahubiri wakosa,     na waliopotea,    wokovu u wake Bwana,     aliyewafilia. 4. Astahiliye hapana    kutamka habari,     lakini Wewe waweza     kutufanya tayari    Neno lako tulijue,    tupe na Roho wako,    ...

75. Mikononi mwa Mitume

1. Mikononi mwa mitume     kazi ilifanywa,     si nguvu yao    walipewa msaada, ndiye Roho.    Wakapata kuona upya tena.        /:Nenda, (kazini tu)         nenda, (siache)         kuyasema.:/         Sisi ni badala yao.          Mitume wa zamani          tupe vipawa vya kazi,         /: tuifanye (tuifanye)         kazi yako (kazi yako):/          ututume, ututume,         ututume  2. Tuombe kupata Roho     tuende kazini.    Si nguvu yetu     kwa kufanya kazi hii    njema mno.     Tutakwenda haraka     kuifanya.          Nenda, nenda … 3. Vuvia Roho Mtakata    ...

76. Mwana Kondoo Ayalipa

1. Mwana Kondoo ayalipa     madeni ya dunia.     Ayachukua makosa     ya wakosaji wote.     Aenda na kuugua,     anakubali kuchinjwa,    furaha aziacha.     Wanamhukumu wampiga,    wanamtukana wamtesa,     asema: Nakubali. 2. Mwana Kondoo ni Mwokozi     ni Mponya wa mioyo;     aliyetumwa na Mungu     awakomboe watu.     Mwanangu, nenda okoa     watoto  niliotupa.     Sababu ya makosa.     Dhambi zao ni nyingi mno;    watolee ukombozi    damu na mwili wako. 3. “Tayari mimi, Babangu,      nitwishe nichukue.      Maneno uyasemayo      nitafuata yote”.     Pendo hili kubwa sana,      lamshika Baba wa mbingu      amtoe mwana wake.     Pendo hili li...

77. Mwana Kondoo wa Mungu Waiondoa Dhambi

1. Mwana Kondoo wa Mungu    waiondoa dhambi;     Tuhurumie. 2. Mwana Kondoo wa Mungu    waiondoa dhambi;    Tuhurumie. 3. Mwana Kondoo wa Mungu     waiondoa dhambi;    Ututulize. Amen.

78. Mwokozi Wangu Umekosa Nini?

1. Mwokozi wangu     umekosa nini?    Wahukumiwa kama mwuaji.    Umeshtakiwa makosa     mangapi uliyotenda? 2. Wapigwa sana,     miiba taji lako,    umetemewa    mate, watukanwa,     wanyweshwa nyongo     tena siki kali,     wasulibishwa. 3. Sababu gani     unateswa hivi?     Makosa yangu     yanakuumiza;    mateso haya yako yanipasa,    mimi mkosaji. 4. Ajabu kubwa     sana tendo lako;     Mchungaji unateswa kwa     ajili ya kondoo,    Bwana     unawalipia watumwa wako. 5. Tulipokuwa mateka     wa mwovu,    nawe ukaja ukatukomboa.    Tulistahili kufa kwa     milele,    ukatufia. 6. Mwokozi wangu    nifanyeje mimi,    niitangaze pote sifa yako? Na-...

79. Nakusalimu Kichwa

1. Nakusalimu kichwa    kilichojaa  damu,     kilichovikwa taji     la miiba mikubwa,     kilichopata enzi    kwa Mungu mbinguni,     kitukanwacho sasa     matusi makali. 2. Naona uso wako     watemewa mate,     heshima yako yote     imeondolewa.    Mwanga wa macho yako     wazimika sasa.     Aliyekuharibu hivi,    ndiye nani? 3. Mateso yako Bwana,    yanipasa mimi.    Wewe waadhibishwa     kwa ajili yangu.     Hukumu unapata     iliyonipasa.    Bwanangu nakuomba,     unihurumie! 4. Na mimi nasimama    msalabani pako;    niwe karibu kwako     utoapo roho;     ukiugua sana    kwa teso la kufa,     nitakushika Bwana     ...

80. Liko Neno Moja Nipendalo

1. Liko Neno moja nipendalo,     ni chakula cha moyo;    Neno hili linanituliza    nikipatwa na shida:     Kumtazama Bwana wetu pale,    atoapo jasho kama damu,    akubalipo mzigo,     Baba aliomtwika. 2. Siku zote  namkumbuka  yeye,     alivyosulibishwa,     akivumilia taabu kimya     kama mwana wa kondoo.    Nami akanikumbuka mimi,    akisema: Yamemalizika!     Huko aliniteka,    nami niwe mtu wake. 3. Bwana wangu,     u mwenye huruma,     mimi ni mkosaji tu;     nilipokuwapo penye giza    wewe ukatokea,     ukamtafuta kondoo wako,    kabla mimi sijakusikia.    Watoa ukombozi unipao uhuru. 4. Ndimi huru lako, Bwana Yesu,    wewe ndiwe Bwanangu.     Jina lako, bora liung’aze moyo  ...

81. Ulimwengu Tazama

1. Ulimwengu tazama,    Yesu Mwokozi wako     asulibiwavyo.     Mwenye heshima yote     anayavumilia    mateso tena matusi. 2. Karibia tazama     maungo yake yote     yatokavyo damu.    Na moyo wake mwema     kwa shida na uchungu     unaugua vigumu. 3. Nani akupigaye,     aliyekufanyia     mambo kama haya?     Wewe huna makosa     kama wengine wote,    hujui kosa lolote. 4. Makosa yangu mimi     yaliyo kama mchanga,     hayahesabiki,    ndiyo yakutiayo     mateso na uchungu      uliyoyavumilia. 5. Mimi nimestahili     kulipa haya yote,     na kufungwa sana.     Mapigo na mateso     uliyopata wewe    yalitoka kwangu mimi. 6. Umejitwika mzigo ...