71. Wajibu Mwema Watoka Kwako
1. K: Wajibu mwema
watoka kwako,
Bwana mwenye
utukufu.
Neno jema ndilo
Jina lako.
W: /: Yesu ni mwanzo
wa kazi shambani,
tena ni Bwana,
wa nguvu kwa utume
wetu.:/
2. K: Watendakazi mwako
shambani,
uwape matumaini.
Nazo nguvu wakiwa
kazini.
W: /: Watende yote kwa
uaminifu,
wawe makini,
huduma isiharibike. :/
3. K: Wapate heri
kuyasikia uliyoyaagizia.
Waje nao kutuhubiria.
W: /: Tena kazini
wakaelezee Neno
kwa wazi, na kweli
ya uzima wako. :/
4. K: Wajihadhari
wawe na hamu,
kushika na kufahamu.
Jina lako likawarehemu.
W: /: Ni wachungaji,
wajue hilo tu
si watawala.
Bwana, ujifunue kwao.:/
5. K: Unawatuma
katika kundi,
kwa bidii na juhudi.
Nasi kwao tuwe mashahidi.
W: /: Ushangiliwe
kwa neema yako,
na kundi lako
lijue lina viongozi. :/
Comments
Post a Comment