132. Roho Mtakatifu Mungu Wetu

1. Roho Mtakatifu, Mungu wetu,

   mtuliza mioyo shidani,

   watumwa toka mbinguni 

   na Mungu Baba na Mwana, 

   Roho Mtakatifu Mungu wetu.

 

2. Roho Mtakatifu, Mungu wetu,

   uwashe moto wa pendo, 

   tupende Neno la Mungu 

   na kupendana na ndugu.

       Roho Mtakatifu …


3. Roho Mtakatifu, Mungu wetu,

   jaza tegemeo letu! 

   Pasipo msaada wa Roho

   hakuna kutegemea.  

        Roho Mtakatifu …


4. Roho Mtakatifu, Mungu wetu,

   twaomba kwako ushujaa 

   wa kupigana na adui  

   mpaka tufike kwako juu. 

        Roho Mtakatifu …


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya