18. Umati wa Yesu
1. Umati wa Yesu,
njooni kwa furaha
msikie habari ya sikukuu!
Mwana wa Mungu
azaliwa kwetu.
Njooni tumtukuze!
Njooni tumtukuze!
Njooni tumtukuze!
Yesu Kristo!
2. Mbinguni malaika
wamwimbia wote
na wote wakaao kwake
Mungu.
Mungu ni mkuu,
aliyetupenda.
Njooni tumtukuze! …
3. Tumsifu Mwokozi
Yesu siku zote,
aliyezaliwa kwetu leo.
Anatujia atufurahishe.
Njooni tumtukuze! …
Comments
Post a Comment