22. Yesu Kitoto Kizuri
1. Yesu kitoto kizuri,
umetujia watoto
utupe mioyo mizuri,
tuwe watoto wa Mungu.
2. Ee Mwanga toka
mbinguni,
umetufikia sisi,
tupate mwanga wa kweli,
tuunganishwe na Mungu.
3. Mpenzi wangu Mtakatifu,
umezaliwa duniani:
furaha iko kwa wote,
kwa wakubwa na wadogo.
4. Unibariki ni mdogo,
moyo unisafishie,
ondoa taka ya roho,
upendo wetu uzidi!
Comments
Post a Comment