27. Amezaliwa Mtoto
1. Amezaliwa mtoto
mjini Bethlehemu.
Nimemchagua yeye,
niwe mali yake!
Oye, oye, niwe mali yake!
2. Nataka kuingia
pendoni mwake yee
na kumtolea moyo
hata vyangu vyote,
Oye, oye, hata vyangu vyote.
3. Kwa moyo wote safi
nataka kumpenda
shidani, furahani
hata kila wasaa.
Oye, oye, hata kila wasaa.
4. Unikubali hivyo,
naomba kabisa
nikuishie Wewe,
leo na daima!
Oye, oye, leo na daima!
Comments
Post a Comment