4. Fungua Milango Yote

1. Fungua milango yote,
  yuaja Bwana wa mbingu.
  Mfalme wa wafalme wote,
  Mwokozi wa ulimwengu.  
  Atuletea uzima;
  kwa hiyo tumwimbieni:
  Tumsifuni Mungu,
  aliyetuumba.

2. Ni mwenye haki na shujaa,
   upole mwingi amevaa;
   Rehema ni taji yake,
   huruma ni fimbo yake:
   Atuondolea shida.
   Kwa hiyo tumwimbieni:
   Tumsifuni Mungu,
   Mwokozi wetu mkuu.

3. Miji na nchi huchipushwa,
   afikako Mfalme huyu;
   nayo mioyo huchekeshwa,
   anayoingia Yesu.
   Ndiye jua la furaha
   linalotufurahisha.
   Tumsifuni Mungu
   mtunza mioyo yetu.

4. Fungua milango yote!
   Tengenezeni mioyo!
   Makuti yawe upole,
   furaha, pendo, amani.
   Mwokozi atawajia,
   aleta raha, uzima.
   Tumsifuni Mungu,
   ni mwenye rehema.

5. Njoo, Mwokozi wangu Yesu,
   nakufungulia moyo.
   Uingie na rehema,
   nione upole wako. 
   Uniongoze kwa roho,
   nifike kwako mbinguni.
   Jina lako Bwana
   lisifiwe pote.

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya