67. Nyesha Mvua

1. Nyesha mvua, nyesha mvua,

   wewe Roho wa Baba,

   nchi kavu ikanyweshwe, 

   imsifu Mungu wetu!


2. Vuma sana, vuma sana 

   Roho mwenye uzima, 

   tulio na usingizi

   utuamshe kwa mkono!


3. Toa mwanga, toa mwanga,

   Roho kwani unang’aa

   wewe ushinde usiku 

   tusikae na giza.


4. Sikiliza, sikiliza,

   wewe Mfalme wa mbingu!

   Tuma Roho wako kwetu, 

   kote kuwe na upya! 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya