75. Mikononi mwa Mitume
1. Mikononi mwa mitume
kazi ilifanywa,
si nguvu yao
walipewa msaada, ndiye Roho.
Wakapata kuona upya tena.
/:Nenda, (kazini tu)
nenda, (siache)
kuyasema.:/
Sisi ni badala yao.
Mitume wa zamani
tupe vipawa vya kazi,
/: tuifanye (tuifanye)
kazi yako (kazi yako):/
ututume, ututume,
ututume
2. Tuombe kupata Roho
tuende kazini.
Si nguvu yetu
kwa kufanya kazi hii
njema mno.
Tutakwenda haraka
kuifanya.
Nenda, nenda …
3. Vuvia Roho Mtakata
ndani mioyoni utuhuishe
tupe moto wa Roho,
tusimame
tuwe tayari kwenda
kutumika.
Nenda, nenda …
Comments
Post a Comment