86. Roho Yangu Tua Hapa
1. Roho yangu tua hapa
mlimani pa Golgota,
angalia tendo hili,
afanyalo Mfalme mkuu.
Amevutwa na upendo
kuacha enzi yake.
2. Yesu alivyotupenda,
twaona msalabani,
maumivu hata manza
ya makosa yampata.
Anakaa mahali petu,
sikia ateswavyo!
3. Kufa kwako kunivute
nife pamoja nawe
mwili na mapenzi yangu
yazikwe nawe Bwana.
Niwe na kutengemana,
mwenye pendo la kweli!
Comments
Post a Comment