10. Bwana Anakuja
1. Bwana anakuja
twendeni kumlaki,
Bwana Mungu wa
majeshi.
Iwasheni mioyo
tukampokee,
huyo Mwenye utukufu.
/:Karibu Bwana, njoo:/
Shinda pamoja nasi.
2. Wewe ndiwe Mfalme, Mfalme
wa mbinguni,
utulishe wenye njaa.
Wewe ndiwe mwanga,
sisi tu vipofu,
tufanye tuone tena.
/:Karibu Bwana...
3. Wewe ndiwe njia,
tutakufuata,
turudi kwa Baba yetu.
Wewe ndiwe kweli,
utuangazie,
tusije tukapotea.
/:Karibu Bwana...
4. Hosana, Hosana,
huyo mbarikiwa,
anakuja kwetu sisi.
Aja kutulisha
na kutugawia
matunda ya ukombozi.
/:Karibu Bwana...
Comments
Post a Comment