100. Mungu Tusaidie
1. Mungu tusaidie,
sisi tunaangamia.
Nchi imeharibiwa
na mwovu wake Shetani.
Kweli kweli ndiye Yesu
aliyewambwa mtini
penye mlima wa Golgotha
aokoe wenye dhambi.
2. Kaonyesha huruma,
Wayuda wakamsumbua.
Wakampiga makofi,
Pilato aliamua.
Kweli kweli ndiye Yesu …
3. Yesu mwenye upendo
alikubali kuuawa,
damu ilimwagika
ili sisi tuokoke.
Kweli kweli ndiye Yesu…
4. Pale msalabani,
Bwana Yesu aliteswa
mzigo wa dhambi zetu
ulimwangukia yeye.
Kweli kweli ndiye Yesu…
5. Sote na tukumbuke,
kifo cha Mwokozi wetu.
Alisema ya kwamba
jililieni wenyewe.
Kweli kweli ndiye Yesu…
6. Habari zilisemwa.
Mahali hapa hayupo,
ona alipokuwa,
jiwe limeondolewa.
Kweli kweli ndiye Yesu…
7. Ni ajabu kabisa
wingu kuja kumpokea.
Habari ilisema
Yesu atarudi tena.
Kweli kweli ndiye Yesu…
Comments
Post a Comment