101. Moyo Wangu Amka Hima
1. Moyo wangu amka hima,
jua limetokea.
Ondoka usingizini,
mpokee Mponya wako,
atokaye kaburini,
kashinda nguvu za kifo, watu
wafurahishwe.
2. Fufuka pamoja naye,
uyaache mabaya!
Maliza mwenendo wako
ukimngojea Yesu,
aliyekwenda mbinguni.
Kwa hiyo nawe ufanye
yampendezayo yeye.
3. Ukiwa na wasiwasi
Yesu anauweza:
Ukipatwa na huzuni,
Yeye furaha yako.
Umtwike Bwana mizigo.
Usisumbuke: yu hapa,
kwani amefufuka.
4. Usimwogope Shetani,
kifo hata kuzimu.
Shida za kufa nyepesi
Mwokozi Yesu ni mzima.
Shujaa wetu haondoki,
awagombea wanyonge
wanaomtumaini.
Comments
Post a Comment