102. Haleluya Tumwimbie
1. Haleluya! Tumwimbie
tumsifu sana Bwana wetu,
tumshangilie kwa shangwe.
Akafungwa na adui
alipokufa msalabani,
lakini sasa yu hai.
Habari njema hii:
Mesiya anakaa mzima kweli.
Haleluya! Tumsifuni!
Tumsifuni Mungu wetu.
2. Haleluya! Tumwimbie,
tumsifu sana Bwana wetu,
tumshangilie kwa shangwe.
Watu wana shida sana,
taabu nyingi na huzuni
mpaka watakapokufa.
Furaha yetu hii:
Bwana ametoka kaburini.
Haleluya! Tumsifuni!
Tumsifuni Mungu wetu!
3. Haleluya! Tumwimbie,
tumsifu sana Bwana wetu,
tumshangilie kwa shangwe.
Atatufufua sisi,
tutafika rahani kwake,
tuishi pamoja naye.
Tumwamini Yeye
Mwokozi wetu mkuu,
mwenye nguvu.
Haleluya! Tumsifuni!
Tumsifuni Mungu wetu!
Comments
Post a Comment