104. Yesu Amefufuka

1. Yesu amefufuka,

   sitakuogopa kufa.

   Amefufuka, naye 

   atanifufua mimi. 

   Atanipa mwili mpya: 

   ni tumaini langu.

 

2. Yesu amefufuka, 

   anapatawala pote. 

   Nami nitatawala 

   pamoja naye milele.

   Atimiza agano:

   ni tumaini langu. 


3. Yesu amefufuka, 

   yanipasa kumngojea. 

   Mwenye kumtegemea 

   Bwana wetu, ataona 

   rehema yake Mungu: 

   Ni tumaini langu.


4. Yesu amefufuka, 

   naweza kumtumikia, 

   nashindana na tamaa, 

   moyo wangu uwe safi. 

   Atanisaidia: 

   Ni tumaini langu.

 

5. Yesu amefufuka, 

   siwezi kutengwa tena 

   na Yesu Bwana wangu, 

   kwa mateso au furaha.

   Vyote  havinishindi:

   Ni tumaini langu. 


6. Yesu amefufuka,

   ni mlango wa kuingia 

   furahani mbinguni.

   Nitatulizwa nikifa, 

   nikiweza kusema:

   U tumaini langu!


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya