107. Kumekucha, ni Mzima

1.  Kumekucha, ni mzima 

    Yesu aliyefufuka. 

    Kaburi lake wazi,

    kufa hakumshiki Yesu.

    Sina woga na kifo, 

    Yesu amefufuka.


2.  Kumekucha, ni mzima  

    Yesu aliyefufuka! 

    Tunaitwa nduguze,

    sababu anatupenda. 

    Tusiachane naye, 

    Yeye aliyeshinda.


3.  Kumekucha, ni mzima 

    Yesu aliyefufuka. 

    Kamba zitufungazo 

    zimekwisha funguliwa 

    Mwili wangu uoze, 

    sina woga na kufa!


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya