11. Natoka Leo Mbinguni

1. Natoka leo mbinguni,

   naleta habari njema 

   habari yenye furaha

   kwa ninyi na watu wote.


2. Amezaliwa kitoto,

   na mwanamwali Maria,

   ni mtoto mzuri na mwema,

   awaletea furaha.


3. Ni Yesu,

   Mwana wa Mungu, Mwokozi

   wa ulimwengu, 

   Atakayekuondoa

   makosa yote na shida.


4. Awapa wote wokovu, 

   uliowekwa na Mungu, 

   mkae nanyi mbinguni 

   pamoja nasi milele.


5. Alama yenu iwe hii: 

   Zizini mtoto maskini 

   aliyevikwa viguo,

   naye ni Bwana wa mbingu.


6. Tumsifuni sisi sote,

   tuwafuate wachunga, 

   tuyaone yale makuu, 

   tuliyopewa na Mungu.


7. Yesu unipendezaye, 

   ugeuze moyo wangu, 

   uwe nyumba yako nzuri, 

   nisikuache daima.


8. Tumsifu Bwana wa mbingu,

   aliyemtoa Mwanawe. 

   Tumwimbie kwa furaha,

   pamoja nao malaika. 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya