110. Haleluya, Haleluya

1.  Haleluya, Haleluya,

    Sauti na mioyo juu, 

    tumwimbie Mungu nyimbo,

    tumsifu na furaha, 

    Aliyemwaga damuye

    kwa ulimwengu wote,

    amefufuka kifoni 

    sasa Yesu Mwokozi.


2.  Minyororo yake kifo 

    imekatika pia,

    na katika wafu wote

    Yee mzaliwa wa kwanza Yesu 

    ameshinda sasa, 

    nasi twashinda naye. 

    Ametupatia nasi 

    uzima wa milele.


3.  Kristo afufuka kwanza 

    nao wengi baadaye. 

    Atakapokuja tena, 

    watatokea naye, 

    mavuno yatakuwako

    mwisho wa ulimwengu, 

    watafika furahani

    wote watakatifu.


4.  Mwokozi amefufuka,

    nasi tutafufuka.

    Tunyeshee kama mvua 

    neema yako ee Bwana. 

    Tutafute yaliyo juu,

    siyo ya ulimwengu,

    na uzima tutapewa

    naye Kristo kwa Mungu.


5.  Tumsifuni, tumsifuni

    Mungu wetu, apaswa. 

    Tumsifuni na Mwokozi, 

    aliyeshinda vita. 

    Tumsifuni naye Roho, 

    kisima cha mapenzi. 

    Tumsifuni Mungu wetu, 

    ni Utatu wa enzi.


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya