112. Leo Siku ya Furaha

1.  Leo siku ya furaha, 

    kila mtu ashangilie, 

    Kristo Yesu afufuka, 

    ateka adui wote! 

    Haleluya!

        

2.  Nyoka wa kale na kifo, 

    kuzimu hata ubaya 

    vimeshindwa na mshindaji Yesu 

    Kristo Mfalme wetu! 

    Haleluya!


3.  Mateka yote ya kifo

    yamekamatwa na Yesu, 

    na ufu umenyang’anywa naye

    aliyefufuka! 

    Haleluya!


4.  Adui hawatushiki 

    tunakwenda uzimani,

    tunapokunywa naye 

    kinywaji kipya milele!

    Haleluya!


5. Jua na mwezi na nchi, 

   viumbe vyote vya Mungu 

   vinafurahiwa leo:

   Mfalme wa uongo ashindwa!

   Haleluya!


6. Kwa hivi tushangilie,

   tumwimbie Yesu Kristo, 

   Yeye ametuokoa,

   afufuka kaburini! 

   Haleluya!


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya