114. Amefufuka Katika Wafu
1. K: Amefufuka katika wafu,
akiwa na utukufu.
Kristo pekee,
ndiye mwenye nguvu.
W: /:Yeye limbuko
la waliolala,
tena ni mwisho
wa nguvu ya mauti
kwetu. :/
2. K: Hii ni habari iliyo kweli,
iletayo udhahiri.
Yapasa wote,
tuache mashaka.
W: /: Yesu usifiwe,
Wewe pekee ndiwe
ustahiliye kushika
mamlaka yote. :/
3. K: Kristo u Bwana
mwenye uweza.
Shetani umemshinda,
kazi yote umeimaliza.
W: /:Uhimidiwe,
Ewe Bwana pekee,
Utupokee tunapokuja
kwako, Bwana.:/
4. K: Tuutangaze ushindi wake,
mataifa waje kwake,
wafahamu utukufu wake.
W: /: Asante, Bwana,
kwa ushindi wako
kwa watu wako.
Shetani hana nguvu
tena.:/
Comments
Post a Comment