119. Bwana Amefufuka, Haleluya
1. Bwana amefufuka, Haleluya.
Tuimbe na malaika, Haleluya.
Sifa zetu na shangwe, Haleluya.
Na zao zisitengwe. Haleluya.
2. Ukombozi timamu, Haleluya.
Umetimu kwa damu, Haleluya.
Mshindi asifiwe, Haleluya.
Yu hai kwa milele, Haleluya.
3. Jiwe, lindo, muhuri, Haleluya.
Vi wapi? Na kaburi? Haleluya.
Kifo hakimuwezi, Haleluya.
Ametoka kuzimu, Haleluya.
4. Yu hai mtukufu, Haleluya.
Cha kifo hatuhofu! Haleluya.
Alitufia sisi, Haleluya.
Tuwe huru na sisi, Haleluya.
5. Kichwa chatangulia, Haleluya.
Tupate, nasi pia! Haleluya.
Kwa kuwa tuna fungu, Haleluya.
Mti, kaburi, mbingu, Haleluya.
6. Ndiwe Mwokozi wetu,
Haleluya.
Sifa ni yako Yesu, Haleluya.
Utukuzwe pekee, Haleluya.
Ni wewe Ufufuo, Haleluya.
Comments
Post a Comment