12. Njooni, Tumheshimu Yesu
1. Njooni, tumheshimu Yesu,
tumtolee sifa zetu.
Tumwimbie kwa furaha,
sisi watu wa Yesu.
2. Baba amemtuma Mwana
atuletee uzima,
utakaopewa watu
wenye shida na kufa.
3. Moyo wake watupenda
kwa upendo amekuja,
aokoe wenye dhambi
wasishindwe na mwovu.
4. Nuru imetutokea,
Yesu akiponda kichwa
cha adui wetu mkali
anayetudanganya.
5. Tutabarikiwa kweli,
tukishika Neno hili,
tukimsifu Bwana Yesu
kwa vinywa na mioyo.
6. Mwana mzuri Bwana Yesu,
twakuomba tupeleke
pale wakuimbiapo
malaika nyimbo nzuri.
Comments
Post a Comment