121. Mwokozi Wetu Amepaa
1. Mwokozi wetu amepaa
mbinguni kwake Baba!
Neno hili ni faraja,
kwa wote wenye woga
Kikiwa kichwa mbinguni,
hata viungo vyafika
alikokwenda yeye.
2. Mwokozi wetu amepaa
mbinguni, mwenye nguvu.
Mbinguni nitapokewa
nitengemane kweli.
Sababu hii ninataka
kufika pale alipo
Mwokozi wangu Yesu.
3. Mwokozi wetu amepaa
mbinguni! Nakuomba:
Bwanangu nisaidie
nikutegemee wee.
Nikufuate daima,
mwisho nifike kwako juu
nikiacha dunia.
Comments
Post a Comment