122. Shujaa Mkubwa
1. Shujaa mkubwa,
Bwana wetu,
leo umejikalisha
kitini kwa Babako.
Ufalme wote ni wako,
umeshinda maadui, hawana
nguvu tena. Umepewa enzi
kubwa, kufa pia na uzima,
vyote unavitawala.
2. Malaika wote
wa mbingu
wanakusifu kwa nyimbo
wanakutumikia.
Ulipotoka mbinguni
ukaja kutuokoa,
na umerudi leo.
Sasa, wako utukufu;
nasi tunakushukuru,
tunasifu Jina lako.
3. Twataka kutafuta tu
ufalme wako wa mbingu.
Utupe nguvu zako,
tushike mwenendo mwema,
tusiwe wenye kiburi
ila wanyenyekevu.
Tuepuke kila kosa,
tufuate njia yako
ya kuingia mbinguni.
4. Yesu mwana wa Daudi
uliyetupatanisha
na Bwana Mungu wetu.
Ulipokwenda mbinguni
umetutengenezea makao ya milele.
Tuongoze, tusichoke,
tusafiri siku zote;
kwani watungoja kwako.
Comments
Post a Comment