123 - Siku Hii Tuliyomwona
1. Siku hii tuliyomwona
akipaa juu mbinguni,
alifia wakosaji,
karudia enzi yake.
2. Huko shangwe yake nyingi
milangoni pa milele.
Kashinda makosa, kufa, Yeye
Mfalme mwenye nguvu.
3. Ajapokwenda mbinguni,
alipenda ulimwengu.
Akikaa kitini mwake,
sisi atutunza hapa.
4. Tazama mkononi mwake
alama za pendo lake!
Awatia mibaraka watu
na makundi yake.
5. Na sisi atuombea
akikaa utukufuni,
na atutengenezea
makao tukae naye.
Comments
Post a Comment