125. Tazameni, Anapaa

1. Tazameni, anapaa, 

   mwenye kushinda vita; 

   gari lake ni mawingu, 

   ndipo anapopita;

   malaika wa mbinguni

   wakimwimbia Bwana; 

   Amekaribishwa sasa, 

   kwa kufurahi sana.


2. Ni nani anayepaa, 

   wote  wakimsifu? 

   Ndiye Bwana mwenye enzi, 

   ndiye Mungu wa Safu,

   aliyeteseka kwanza 

   mle katika mti,

   kwa kifo chake mwenyewe,

   akashinda mauti.


3. Akaaga watu wake, 

   na akawabariki 

   akapaa mawinguni 

   na wakimwangalia,

   chini hutenda ya Mungu, 

   yote yakatimia;

   kazi yake imekwisha, 

   kwake amerejea.


4. Ni Kuhani wetu sasa, 

   yumo na damu yake,

   katika patakatifu 

   twapatanishwa kwake; 

   Amefanya ukombozi 

   kuondoa dhambi zetu; 

   Mungu amemkubali 

   ndiye sadaka yetu.

 

5. Mwili ameuinua

   huo wa ki-Adamu, 

   ndani yake sisi sote  

   pia tuna sehemu,

   Mungu na Mtu pamoja, 

   yuko huko enzini

   twaamini Bwana, 

   kwamba

   tutakwenda mbinguni.


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya