127. Karibu kwangu Roho
1. Karibu kwangu Roho
ingia moyoni,
uliyeniletea uzima na raha.
Roho Mtakatifu wa Baba na wa Mwana
ufananaye nao ukaaye nao.
2. Unafundisha watu
kuomba vizuri,
wapate kusikiwa
na Mungu mbinguni.
Unatuombea, hukomi,
mpaka Mungu atende
mambo yale uliyoyaomba.
3. Wafurahisha moyo,
hupendi huzuni;
tukiwa matesoni, unatutuliza.
Wazungumza nasi
kwa Neno lako tamu,
unatia mioyo furaha ya kweli.
4. Unatufanya sisi kuwa usharika;
hutaki tugombane
na kuchukiana.
Wanaopigana unawapatanisha;
wataka wapendane
Wakristo wowote.
5. Ulinde nchi yetu, serikali yetu,
tukae na amani duniani humu.
Uwape wakubwa,
pamoja na wadogo
uchaji na akili,
wampendeze Mungu.
6. Katika mwendo wetu
utupe na sisi nguvu,
tumshinde mwovu akitujaribu.
Utusaidie, tushike njia yako
na mwisho tufe vema
tufike kwa Mungu.
Comments
Post a Comment