128. Roho Mtakatifu Uje

1. Roho Mtakatifu uje 

   utukalie na sisi, 

   fanya makao kwetu.

   Utupe nuru ya mbingu, 

   ung’aze mioyo yetu, 

   tumtumikie Mungu. 

   Uje, lete utukufu 

   na furaha na uzima;

   haya twatafuta kwako.


2. U chemchem yenye rehema,

   unatunywesha hekima, 

   watufundisha vema, 

   tujue kuwaambia 

   wenzetu wasiojua 

   habari za wokovu.

   Roho zetu uzifunge,

   tuyatende mambo mema 

   wewe utukuzwe sana.


3. Umande mzuri wa mbingu,

   geuza mioyo yetu, 

   tujae pendo lako.

   Tupendane na wenzetu,

   tuwafanyie mema tu

   na kweli watu wote.

   Kwetu uwe upendano; 

   kugombana kuwe mbali, 

   tuwe na amani daima.


4. Ututakase mioyo, 

   utupe nguvu rohoni, 

   tushike mwendo mwema. 

   Tusifuate kiburi,

   tamaa mbaya za mwilini 

   na mambo ya dunia.

   Roho zetu ziongozwe 

   zifikiri mambo yako, 

   mpaka tufikapo kwako. 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya