129. Twaomba Roho wa Mungu

1. Twaomba: Roho wa Mungu

   Mfariji wetu mkuu, 

   utupe baraka.

   Yesu alipotuaga, 

   kasema:  Namtuma 

   Roho wangu kwenu.

 

2. Utuamshe wakosaji 

   kwa kuwa tu kondoo

   waliopotea.

   Uokoe ulimwengu, 

   umeharibika, 

   upate kujuta.


3. Roho wa ujuzi mwingi, 

   fundisha Wakristo 

   wampendeze Mungu. 

   Utufundishe kuomba

   kwa Mungu vizuri,

   tusikiwe naye.


4. Utusaidie sana, 

   tumshinde Shetani 

   na dunia pia.

   Tusitengwe na Mwokozi, 

   yakija mateso, shida na huzuni


5. Twakuomba uwe nasi 

   tulio wanyonge tukijaribiwa.

   Mwisho tutakapokufa, 

   tuone furaha baada ya mateso.


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya