13. Salamu, Yesu Bwanangu
1. Salamu Yesu Bwanangu, Wewe
uzima wangu.
Nimekujia naleta
vyote ulivyonipa:
Ni moyo na mwili wangu, hata
na mawazo yangu,
ndiyo heshima yangu.
2. Umezaliwa Bwanangu
kwa ajili ya mimi;
umenipenda kabisa,
umenipa wokovu.
Tangu mimi sijaumbwa,
umenitengenezea,
ukombozi wa moyo.
3. Uvuli mzito wa mauti,
ulinifunikiza:
Umenitokea jua,
waniangaza moyo.
Wewe Bwana umenipa nuru,
raha na uzima.
Nakushukuru Bwana.
Comments
Post a Comment