130. Ee Roho Uje
1. Ee Roho uje, ee Bwana,
ujaze kipaji chako,
kwao uliowakusanya
washa moto wa upendo!
Umetuita mwangani,
tuwe umoja pendoni,
tulio wa ulimwenguni,
kwa hiyo daima twakusifu.
Haleluya, Haleluya!
2. Mtuliza moyo Mtukufu,
tuagize, Neno lako
litufundishe kumtambua
Mungu na kumwita Baba.
Umetuita …
3. Vitani tupe upozi,
kituo cha kutulia,
na tusiogope ukali
wa adui na wa mwili.
Umetuita …
Comments
Post a Comment