133. Uje Roho mwenye Neema
1. Uje Roho mwenye neema,
uje hua wa mbinguni,
lete mwanga wa upozi,
Ee mlinzi na kiongozi!
2. Tuchague njia yako,
kweli twaiona sasa,
ututie woga mwema,
tusimwache Mungu wetu!
3. Tupeleke kwa Mesiya,
Yeye mwanzo wa uzima,
tuyatende mema yote,
ndiye njia ya mbinguni!
4. Tupeleke furahani,
tukapate kupumzika;
tupeleke kwake Mungu,
kwake iko raha bora!
Comments
Post a Comment