135. Bwana Nasikia Kwamba
1. Bwana nasikia kwamba
umebariki wengi,
nami nakuomba sasa:
Nibariki na mimi!
Na mimi na mimi,
Nibariki na mimi.
2. Nipitie Baba yangu,
kweli mimi mkosaji,
Baba uingie kwangu,
nirehemu na mimi!
Na mimi na mimi
Nirehemu na mimi.
3. Nipitie, nakuomba,
Bwana Yesu, Mwokozi,
wakosaji wawaita,
uniite na mimi!
Na mimi na mimi
Uniite na mimi.
4. Nipitie Roho mwema
kweli mimi sioni,
mwenye nguvu za kuonya,
nipe nguvu na mimi!
Na mimi na mimi
Nipe nguvu na mimi.
5. Nipitie Baba yangu,
nakuomba kwa bidii,
umebariki wengine,
nibariki na mimi!
Na mimi na mimi
Nibariki na mimi.
Comments
Post a Comment