138. Tumepokea Neema
1. K: Tumepokea neema,
tuimbe sote kwa
shangwe.
W: Tumepokea neema,
tuimbe sote kwa
shangwe
K: Mungu Baba
kampeleka
Roho Mfariji wake.
W: Mungu Baba kampeleka
Roho Mfariji wake.
K: Ee ndugu,
W: furaha kubwa
K: isiyo
W: na mwisho kweli.
K: Tunao
W: sasa uweza
K: kwa nguvu
W: zake Mwokozi.
2. K: Njoo, Roho Mtakatifu,
utujaze nguvu zako;
W: Njoo, Roho Mtakatifu,
utujaze nguvu zako;
K: Tuende kwa watu wetu,
tutangaze neema yako.
W: Tuende kwa watu wetu,
tutangaze neema yako.
K: Ee ndugu, …
3. K: Ee Roho Mtakatifu,
uliye Mwanga wa kweli,
W: Ee Roho Mtakatifu,
uliye Mwanga wa kweli,
K: Twapenda kukusujudu,
kwani u pamoja nasi.
W: Twapenda kukusujudu,
kwani u pamoja nasi.
K: Ee ndugu, …
4. K: Ahadi ya Yesu Kristo,
hakika imetimizwa;
W: Ahadi ya Yesu Kristo,
hakika imetimizwa;
K: Twaimarishwa mioyo,
tuishuhudie neema.
W: Twaimarishwa mioyo,
tuishuhudie neema.
K: Ee ndugu, …
5. K: Baba Mungu,
naye Mwana,
naye Roho Mtakatifu,
W: Baba Mungu,
naye Mwana,
naye Roho Mtakatifu,
K: Mungu wa Utatu,
Mmoja,
milele tutakusifu.
W: Mungu wa Utatu,
Mmoja,
milele tutakusifu.
K: Ee ndugu, …
Comments
Post a Comment