139. Mungu Atukuzwe Pekee

1. Mungu atukuzwe pekee, 

   shukrani zitolewe

   sababu ya rehema kuu 

   aliyotutendea.

   Mungu atupenda sana, 

   sababu hii ametupa 

   kutengemana vema.


2. Twakutukuza Baba mkuu 

   twakuheshimu sana, 

   sababu ya kutawala

   zamani hata leo.

   Nguvu zako haziishi 

   utakayo yatendeka, 

   Muumba wetu ndiwe.


3. Twakutukuza ee Yesu

   Mwana wa Mungu wetu, 

   Uliyetupatanisha 

   na Baba mwenye enzi. 

   Mwana Kondoo wa Mungu,

   sikia tukikuomba

   Mwokozi wetu ndiwe.


4. Twakutukuza, ee Roho 

   uliyekuja kwetu. 

   Uwape nguvu Wakristo 

   waliokombolewa. 

   Utuokoe shidani. 

   Shetani asitushinde,

   Mtuliza mioyo ndiwe

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya