140. Tumsifu sisi Watu
1. Tumsifu sisi watu,
tumsifu Mungu Baba,
aliyeumba vyote
kwa nguvu yake kuu.
Wazima watu wote,
na ndege wa angani
wanyama wa mwituni,
kwa huruma yake.
2. Tumsifu sisi watu,
tumsifu Bwana Yesu,
aliyetukomboa
kwa damu yake tu.
Amani tumepewa,
hatuna hofu tena
Ametuhurumia,
Mwokozi ni yeye.
3. Tumsifu sisi watu,
tumsifu Roho, ndiye
mtulizaji popote,
furaha iwe kuu.
Moyo umetulia,
amani umepata.
Awatakasa wote,
wamwombao yeye.
Comments
Post a Comment