16. Tunakuamkia Yesu
1. Tunakuamkia Yesu,
tunakupa pongezi.
Umezaliwa kikiwa,
malaika wakuabudu,
Uwe nasi!
2. Mwana wa Mungu
wa pekee,
Yeye ni mgeni wetu,
Anajiunga na sisi
Mfalme wa kale na kale!
Uwe nasi!
3. Ashikaye ulimwengu
ashikwa na Maria!
Ni mtoto mdogo na
mchanga!
Tena ni Bwana wa
mbingu! Uwe nasi!
4. Nuru ya milele aja
kuleta mwanga wake.
Aondoa giza lote;
tuwe watoto wa mwanga.
Uwe nasi!
5. Kwetu akawa maskini
kwa kutuhurumia,
tupate mali ya mbingu,
tuwe watoto wa Mungu.
Uwe nasi!
6. Amefanya haya yote
kwa kuwa atupenda.
Kwa hiyo furahini tu
na tumshukuru daima!
Uwe nasi!
Comments
Post a Comment