20. Njooni Wachungaji Bethlehemu!
1. Njooni wachungaji
Bethlehemu!
Njooni kumtazama
mtoto mzuri.
Mwana wa Mungu amezaliwa.
Baba amtuma awakomboe.
Msiogope!
2. Twende Bethlehemu tukaone
tulivyoambiwa na malaika.
Tuyaonayo tutatangaza
na kutukuza kwa nyimbo nzuri
Haleluya!
3. Kweli malaika wametangaza
Furaha kubwa kwa wachungaji.
Sasa po pote patengenezwe,
na watu wote watapendezwa.
Furahini!
Comments
Post a Comment