21. Watoto Njooni Bethlehemu
1. Watoto njooni, Bethlehemu,
njooni zizini kuona makuu
Mungu aliyotutendea leo,
watoto waone furaha kubwa.
2. Twaona kitoto kizuri hapa, wa-
zee wamtazama,
wanafurahi.
Wachungaji wote
wamwangukia,
malaika wa mbingu wanam-
wimbia.
3. Pigeni magoti na wachungaji!
Wakubwa, wadogo
tumnyenyekee!
Tuimbe na sisi kwa
furaha kuu, nyimbo za
kumsifu Mwokozi Yesu!
4. Watoka mbinguni utuokoe,
waona uchungu sababu yetu,
leo wazaliwa mwana kikiwa.
Halafu wateswa, unatufia.
5. Twapenda kukupa mioyo yetu,
twataka kukutumikia vema.
Takasa mioyo ikupendeze,
tupate kufika kwako
mbinguni.
Comments
Post a Comment