23. Msifuni Mungu, Wakristo
1. Msifuni Mungu, Wakristo,
aliyetukuka,
atufungulia mbingu
/:kumtoa mwanawe:/
2. Atokaye kifuani
pa Mungu Babaye,
alala sasa kitoto
/: kitupu, maskini. :/
3. Anyonya kwa mama yake,
maziwa chakula,
kwa kweli anatulisha
/:chakula cha mbingu.:/
4. Ageuza hali yake,
avaa mwili wetu
na sisi anatuvika
/: uzima wa Mungu. :/
5. Akawa mtumwa, na mimi
naitwa kibwana,
niwe nduguye na mtoto
/: wake Mungu Baba :/
Comments
Post a Comment