24. Ulimwenguni Pote

1. Ulimwenguni pote

   asifiwe Mungu mkuu 

   amemtuma Mwokozi, 

   wakosaji wapone.


2. Zamani wazee wale 

   wameona hamu kuu, 

   waondoshwe makosa 

   na kumpata Mwokozi.


3. Abrahamu, Yakobo

   na watu wa Sayuni 

   walimngojea sana, 

   sasa ametujia.


4. Karibu Mponya wangu 

   niondolee woga.

   Ujitengenezee

   njia moyoni mwangu.


5. Safisha nyumba yako 

   umfukuze Shetani, 

   yule nyoka wa kale.

   Nikutumikie wee!


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya