25. Mungu ni wa Utukufu

1. Mungu ni wa utukufu 

   panapo mbinguni juu, 

   na kwao wampendezao 

   duniani raha kuu. 

   Sikieni nchi zote 

   huko mjini Bethlehemu: 

       /: Kristo amezaliwa,   

          Bwana wetu daima. :/


2. Watu na malaika wote

   wanamtukuza Yesu, 

   ashukaye toka mbingu 

   kuwa kama maskini.

   Akaacha enzi yake, 

   akavaa unyenyekevu: 

        /: Kristo amezaliwa,.. :/


3. Asifiwe Mungu Mwana 

   na Mwokozi wa watu, 

   mleta mwanga na uzima 

   Yesu mshinda kuzimu, Mfalme

   wa utengemano 

   huko mjini Bethlehemu.

       /:Kristo amezaliwa, ...:/ 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya