30. Mpige Mbio, Wachungaji

1. Mpige mbio, wachungaji  

   mpige mbio wote, 

   Chukueni na filimbi na 

   zumari pia.

   Mpige mbio wote,

   mpige mbio wote 

   Bethlehemu kwenye hori

   walishwamo ng’ombe.


2. Mumtazame mtoto mzuri

   aliyezaliwa,

   na wazazi wake mtoto 

   wako huko naye.

   Ni Yosefu baba 

   na Maria mama,

   mwanamwali mzuri sana

   kama malaika juu.


3. Hebu njooni, ee jamani 

   mlete nguo nzuri!

   Tumlazeni mtoto wetu

   kwa uzuri wote! 

   Twakubembeleza 

   wewe mtoto lala! 

   Lala Yesu mpenzi wetu 

   twakubembeleza.

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya