31. Malaika Njooni Toka juu!
1. Malaika njooni toka juu!
Oye, oye, tazama,
tazama kitoto.
Imbeni, pigeni panda.
Haleluya! Haleluya!
Nyimbo za Yesu na Maria!
2. Kwa sauti kuu mwimbieni!
Oye, oye, tazama,
tazama kitoto.
Kwa vinanda na vinubi.
Haleluya! Haleluya!
Nyimbo za Yesu na Maria!
3. Tungeni nyimbo tamu mno,
Oye, oye, tazama,
tazama kitoto,
kupita ndege wa anga.
Haleluya! Haleluya!
Nyimbo za Yesu na Maria!
4. Utamu wa nyimbo zenu,
Oye, Oye, tazama,
tazama kitoto.
Umbembeleze, alale.
Haleluya! Haleluya!
Nyimbo za Yesu na Maria!
5. Watu na watengemane,
Oye, oye, tazama,
tazama kitoto.
Na Mungu tumpe
shukrani!
Haleluya! Haleluya!
Nyimbo za Yesu na Maria!
Comments
Post a Comment