34. Wakristo Furahini

1. Wakristo furahini,
   furahini sana! 
   Mwaipigiwa leo 
   mbiu yenu njema! 
   Malaika wanaimba 
   huko juu mbinguni,
   /: wanaimba vizuri 
   sauti ya kushangaa! :/

2. Hivi wanavyoimba: 
   Furahini nyote! 
   Acheni kuogopa, 
   tazameni nyote
   kwani amezaliwa 
   Mwokozi wa pekee:
   /: ni Bwana Yesu Kristo, 
   Mwana Mungu wetu:/

3. Shangilieni nyote 
   na  kusikiliza. 
   Wapigieni nyote 
   mbiu na sauti kuu. 
   Mungu katupa sote 
   mtoto wa mbinguni,
   /: kwa kutupenda sisi 
   amekuja kwetu. :/

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya