37. Sote Tufurahi
1. K: Sote tufurahi,
W: habari ni njema
K: Njooni nyote wahi,
W: tupate uzima
Sasa yametimia
yaliyotabiriwa
Mwokozi kazaliwa.
2. K: Kule Bethlehemu
W: Yesu kazaliwa
K: Mama Mariamu
W: alivyoambiwa. Sasa …
3. K: Kumbe, huyo Mwana
W: kalazwa horini
K: Huyo Yesu Mwana
W: akawa shidani. Sasa …
4. K: Mwana atiiye
W: ni Bwana shujaa,
K: Kwake tuwe wana,
W: ni Mponya dunia. Sasa …
5. K: Jeshi la mbinguni
W: katoa Injili.
K: Watu malishoni,
W: kaona ni kweli. Sasa …
6. K: Mungu yupo nasi
W: katika dunia.
K: Pendo kwa waasi,
W: katoa kwa nia. Sasa …
7. K: Raha na tushike,
W: tunaye Masihi
K: Haya twende kwake
W: sauti zasihi. Sasa …
8. K: Wote wenye Mwana
W: wanao uzima.
K: Yeye ndiye Bwana,
W: atoa karama. Sasa …
9. K: Nyota yatunuka
W: shinani mwa Yese.
K: Bwana atukuka,
W: akatutakase. Sasa …
10.K: Sasa, ndugu, nyote
W: tangaza neema.
K: Waje kwake wote
W: tupate rehema. Sasa …
Comments
Post a Comment