39. Tumezaliwa Mtoto
1. K: Tumezaliwa mtoto,
tumezaliwa mtoto.
Ni Bwana Yesu,
Mwana wa Mungu
Atakayewachunga
kondoo.
W: Amezaliwa mtoto.
Asante, Bwana Mungu.
/: Ulivyoona kondoo wako,
huku chini ya mbingu,
hawana Mchungaji. :/
2. K: Wewe Mama Mariamu,
wewe Mama Mariamu,
Utaziona huzuni nyingi
atakapotimiza sheria.
W: Wewe Mama Mariamu,
na umshukuru Mungu,
/: Alivyoona kondoo wake,
huku chini ya mbingu,
hawana Mchungaji. :/
3. K: Ni furaha yetu kubwa,
ni furaha yetu kubwa,
Tukitumiwa Mwokozi
Yesu ili atupiganie vita.
W: Ni furaha yetu kubwa,
na tumshukuru Mungu.
/: Alivyoona kondoo wake,
huku chini ya mbingu,
hawana Mchungaji. :/
Comments
Post a Comment