40. Tushangilie Sote
K: Tushangilie sote
W: Kila mtu.
K: Mwana wa Mungu
akaja
W: Hata kwetu.
K: Tumjue Mungu Baba
W: Wa huruma.
K: Usiku wa manane
W: Shangwe kubwa
K: Alipozaliwa Kristo
W: Awe Mfalme.
K: Pale katika mji
W: Wa Daudi.
K: Kwenye kondoo hata
ng’ombe
W: Bethlehemu.
K: Na akaitwa kwa Jina
W: La ajabu.
K: Nalo Yesu Mwokozi
W: Mungu nasi.
K: Hakika ni Mwokozi
W: Mwenye enzi
K: Tupatiwe uzima
W: Wa milele.
K: Na kumtumikia daima
W: Siku zote.
K: Maana kwake
sasa tumemwona
W: Mungu wetu.
K: Na hivyo hata Roho
W: Mtakatifu
K: Njoni kwa hiyo
tumsifu
W: Bila mwisho.
Comments
Post a Comment