44. Mjini Mwake Daudi
1. Mjini mwake Daudi
bandani mwa mifugo
mtoto alizaliwa
na mamaye maskini
Mariamu ni mama
Yesu mwanawe mwema.
2. Yesu akawa mbinguni
akatoka enzini
hakukaribishwa chini
akalazwa horini
akaja kimaskini
kuketi duniani.
3. Siku za ujana wake
akimheshimu mama
na kumtii katika yote
kama alivyosema.
Kila mwana na awe
mtii kama Yeye.
4. Amekuwa hata sasa
kielelezo chetu
alikuwa na unyonge
kama unyonge wetu
kucheka na kulia
ni kama sisi sote.
5. Tutamwona waziwazi
ndiyo ahadi yake
sasa aketi mbinguni
katika enzi yake
sote na tumwandame
kwani ni Mfalme wetu.
6. Tutamwona Yeye tena!
Si katika kibanda,
ila juu: na sisi sote,
kwake tutakutana.
Hivyo tutakuwepo
mbele yake daima.
Comments
Post a Comment